Na Seif Mangwangi, Arusha
SERIKALI imewataka wahitimu wa masomo mbalimbali nchini kutumia elimu na ujuzi waliopata kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta watakazoenda kuzifanyia kazi, kuwa wabunifu na weledi na kwamba elimu waliyopewa ndio msingi wa mafanikio yao.
Mwito huo umetolewa leo Disemba 19, 2025 na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Msham Ali Munde katika mahafali ya 27 ya chuo cha uhasibu Arusha yaliyofanyika katika viwanja vya mpira chuoni hapo ambapo wanafunzi wa ngazi za Astashahada, stashahada na Shahada walitunukiwa vyeti vyao.
“Taifa linahitaji vijana kama ninyi: wabunifu, wachapakazi, wanaojifunza kila siku na wanaoweza kutatua changamoto za jamii inayowazunguka, mmeandaliwa vizuri nendeni mkalete mabadiliko katika sekta mnazokwenda kutumikia. Thamani na tija ya elimu yenu mliyoipata vitaonekana endapo tu mtakuwa waadilifu, wabunifu, wazalendo na mtakapojituma katika kazi mtakazoenda kuzifanya katika maeneo mbalimbali kwenye sekta ya umma na binafsi,” amewaeleza wahitimu Mhandisi Mkunde.
Aidha ametoa wito kwa wahitimu kutumia elimu waliopata katika chuo cha uhasibu( IAA ), kama nyenzo ya kujijenga kimaisha na kiteknolojia, kuchochea maendeleo ya familia zao, na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa.
“Mkawe vijana wanaotafuta fursa badala ya kusubiri, mkawe wabunifu katika kutatua changamoto za jamii, mkawe waadilifu katika taaluma zenu, na mtumie maarifa yenu kuongeza tija, ubunifu na ufanisi popote mlipo, ili Tanzania inufaike kupitia kazi zenu, weledi wenu na ndoto zenu zinazotekelezeka,” amesisitiza Mhandisi Mkunde.
Mkuu wa chuo profesa Methew Sedoyeka amesema jumla ya Wahitimu wanaohitimu leo ni 4821 kati yao kati yao wanaume ni 2810 na wanawake 2011.
Amesema chuo kimeendelea kukua na kuongeza kampasi mpya katika mkoa wa Geita jambo ambalo limeendelea kuvutia wanafunzi wengi kujiunga na chuo hicho kwa gharama nafuu.
“Mwaka jana tumesherekea Mahafali ya 26 tukiwa na Kampasi tano ambazo ni Arusha, Babati, Dar es Salaam, Dodoma na Songea. Agosti15, 2025 tulipata ithibati kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) ya usajili kamili wa Kampasi yetu mpya ya Bukombe Mkoani Geita, na imeanza kupokea wanafunzi kuanzia mwaka huu wa masomo; hivyo kufanya chuo kuwa na jumla ya Kampasi Sita,”.
Amesema hiyo imekuwa ni hatua muhimu katika maendeleo ya chuo, kwa kuwa itaongeza uwezo wa chuo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi na kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kunufaika na upatikanaji wa huduma ya elimu ya juu karibu zaidi na kuchangia uchumi wa maeneo yalipo chuo hicho.
Profesa Sedoyeka amesema Chuo cha Uhasibu Arusha kimeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam kwa jamii.
“Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, tumeimarisha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia, kuongeza majengo ya madarasa, maabara za TEHAMA, maktaba za kisasa pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa wahadhiri na wafanyakazi,”amesema.
Amesema pia chuo kimeendelea kupanua wigo wa programu zake za kitaaluma kuanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada ya Kwanza hadi Shahada za Uzamili.
“Katika mwaka huu wa masomo tuna jumla ya kozi themanini na moja (81) kati ya hizo; kozi kumi na tisa (19) ni ngazi ya astashahada /cheti, kozi ishirini (20) ni za ngazi ya stashahada, kozi ishirini na saba (27) ni ngazi ya shahada na kozi kumi na tano(15) kwa ngazi ya shahada ya uzamili,” ameongeza.
Profesa Sedoyeka ametoa wito kwa wahitimu hao kwenda kutumia ujuzi waliojipatia kujiletea maendeleo binafsi, kuinua familia zao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
“ Daima zingatieni maadili, uwajibikaji na uongozi bora katika kila jukumu mtakalokabidhiwa, kwani mafanikio ya kweli hayapimwi kwa cheo au kipato pekee, bali kwa mchango chanya mnaoutoa kwa wengine, mkawe mabalozi wema wa Chuo cha Uhasibu Arusha na mfano bora kwa kizazi kijacho,” alimaliza Prf.Sedoyeka.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la chuo Dkt. Mwamini Tulli amewapongeza wahitimu wote wa mwaka 2025 kwa juhudi, nidhamu na uvumilivu waliouonesha hadi kufikia hatua ya kuhitimu.
“Thamani ya elimu yenu itathibitishwa na namna mtakavyoitumia elimu yenu kuleta maendeleo yenu binafsi,maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla,” amesema.
Amesema ni wajibu wa wahitimu kuwa wabunifu, wenye ujuzi wa vitendo, kuwa tayari kuendelea kujifunza muda wote na kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia katika fani walizosomea.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...