Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe ameshiriki  sherehe ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Jamhuri ya Zambia, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2025. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Maghembe aliwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na aliitakia heri na mafanikio Jamhuri ya Zambia na wananchi wake. 

Mhe. Magembe amesema  maadhimisho ya uhuru wa Zambia, yenye kauli mbiu  isemayo "Kujenga Zambia Imara na yenye Ustawi" inazikumbusha nchi nyingi za Afrika, kuhusu jitihada madhubuti  zilichukuliwa na Zambia wakati wa kupigania uhuru na kuleta maendeleo ya Taifa na Wananchi wake.

Amesema jitihada za Waasisi wa Uhuru  Barani Afrika akiwemo aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zambia Hayati Keneth Kaunda na Hayati Mwalimu Julius Nyerere zimeimarisha uhusiano wa uwili kati ya mataifa hayo na kuweka misingi ya amani na umoja kwa manufaa ya wananchi wao.

Mhe. Magembe ameishukuru Zambia kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia reli ya TAZARA, biashara na uwekezaji ambavyo alieleza kuwa ni utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kati ya mataifa hayo. 

Awali, Balozi wa Zambia nchini Mhe. Matthews Jere alielezea azma ya nchi yake kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na Tanzania katika sekta za elimu, usafirishaji, kilimo, madini na nishati.



















 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...