wadai suluhu ya changamoto haitatuliwi kwa uvunjifu wa amani. 

Na Mwandishi Wetu

Umoja wa  wa Wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam umewataka Watanzania wote kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kuliingiza taifa katika uvunjifu wa amani, wakisisitiza kuwa machafuko hayaleti tija wala suluhu ya changamoto za kijamii na kiuchumi.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam viongozi na wanachama wa umoja huo wamesema wanapinga vikali wito wowote unaotolewa na wanaharakati wa ndani na nje ya nchi wanaohamasisha vurugu kwa maslahi yao binafsi, huku wakilitumbukiza taifa kwenye machafuko na hofu.

Wajasiriamali hao wamesema wamefuatilia kwa karibu matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kubaini kuwa kulikuwa na watu waliokuwa nyuma ya pazia wakihamasisha vitendohivyo.Wamesisitiza kuwa wamewashtukia na wanapinga vikali mienendo hiyo hatarishi.

“Matukio ya Oktoba 29 yametosha kuwa somo. Tumeshuhudia athari zake na tumejifunza kuwa uvunjifu wa amani hauwezi kuleta maendeleo wala suluhu ya amani,” walisema kwa pamoja.Umoja huo umeeleza masikitiko yao makubwa, ukilaaani kwa nguvu zote vitendo vya uchochezi na kuwaasa h vijana wa Kitanzania kutowasikiliza watu wanaohamasisha vurugu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa ndani na wanasiasa wanaotumia fursa hizo kujinufaisha kisiasa na kwa maslahi yao binafsi.

Kwa mujibu wa tamko hilo wamesema waathirika wakubwa wa vurugu za Oktoba 29 walikuwa ni wafanyabiashara, wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga), waliopata hasara kubwa kutokana na uharibifu wa mali na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.

“Tutaendelea kupaza sauti kupinga uchochezi. Tutapingana na wanaharakati wote wanaojificha nje ya nchi kuhamasisha vurugu na maandamano. Tunakataa ushawishi wote wa wanamitandao wanaolenga kueneza chuki. Tutawapinga wanasiasa wote wanaohamasisha vurugu na tutawakemea viongozi wa dini wanaoingiza siasa katika majukwaa ya kiimani,” wameeleza katika tamko hilo.

Hata hivyo, wajasiriamali hao wamesema wataendelea kuwahamasisha vijana wa kizazi cha Gen -Z kuwa nguvu kazi muhimu na kuwa na msimamo wa kulinda taifa, amani na mshikamano wa kitaifa.

Kwa upande wake Mzee Omary Suleiman mfanyabiashara wa Soko la Kinondoni,akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali, amesema vurugu hizo zilitokana na uchochezi wa makusudi na kusisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena.

“Tanzania ni mimi, na mimi ni nchi. Tunaomba Watanzania wote waunge mkono jitihada hizi ili Tanzania ibaki salama, yenye amani na utulivu,” alisema Mzee Suleiman.Tamko hilo limekuja kufuatia ushirikiano wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Raslimali na Taarifai ( MECIRA) imeelezwa kufanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya uraia kwa wafanyabiashara, hatua inayochangia kuongeza uelewa kuhusu haki, wajibu na umuhimu wa kulinda amani ya taifa.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria ni pamoja na Husein Bambe, Kiongozi wa Wajasiriamali Ubungo; Bakari Sufia wa Ilala; na Pelagia Michael, Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Kinondoni, ambao kwa pamoja walisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa biashara, maendeleo na ustawi wa Taifa la Tanzania.

 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...