‎


Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ameziagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwasha mitambo yote ili kuondoa mgao wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani, kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha maji katika Mto Ruvu baada ya hatua za dharula kufanyika katika chanzo mvua takribani milimita 50 kunyesha katika safu za milima ya Uluguru, mkoani Morogoro.

‎Mhe. Aweso ametoa maelekezo hayo mara baada ya kufika katika Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini, uliopo Bagamoyo mkoani Pwani, ambako ameshuhudia Mto Ruvu ukirejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya kipindi cha kupungua kwa kina cha maji.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso ameeleza kwa kina na wazi mipango ya serikali katika dhamira ya kuhakikisha changamoto hii haijitokezi tena kwa uwepo wa Mradi wa Bwawa la Maji la Kidunda linalotarajiwa kukamilika mwaka kesho, sambamba na ujenzi wa awamu ya pili(phase2) ya Mradi wa maji visima vya Kigamboni nikihitimisha na mpango mkakati ambao tayari umefanyiwa upembuzi yakinifu wa Ujenzi wa mradi wa Maji Rufiji.‎

‎Kuhusu malalamiko ya wananchi kubambikiziwa bili za maji licha ya kutopata huduma hiyo, Waziri Aweso ameielekeza DAWASA kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua stahiki dhidi ya watakaobainika kuhusika.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami–Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasi, ameeleza kuhusu kiwango cha mvua kilichorekodiwa pamoja na hatua za udhibiti wa uchepushaji wa maji ya Mto Ruvu, akisema kuwa bodi inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ipasavyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...