Farida Mangube Morogoro.

Watu kumi wamefariki Dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali  ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia leo Januari Mosi 2026 katika eneo la Mwidu Mikese, mkoani Morogoro.

Ajali hiyo ilihusisha basi dogo na lori la mizigo imetokea katika Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Wilaya ya Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, ajali hiyo imetokea baada ya basi dogo lenye namba za usajili T 162 DMD, lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Sherehe Juma, kugongana na lori la mizigo aina ya HOWO lenye namba za usajili T 956 ELU na tela namba T 828 ELW.

Lori hilo ni mali ya Kikori Company, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Abuu mkazi wa Msoga Chalinze, mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 28.

 Dereva huyo alikuwa akisafirisha shehena ya mbolea kutoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya.

Majeruhi wote 18 wamekimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu, ambapo hali zao zinaendelea kufuatiliwa na wataalamu wa afya.

Jeshi la Polisi limethibitisha vifo hivyo na kueleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo, huku likitoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...