*Autaja mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji ya Mvua eneo la Kidete.
WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 02, 2026 amezungumza na wakazi wa Tindiga wilaya ya kilosa mkoani Morogoro ambao wameathirika na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Mheshimi wa Dkt. Mwigulu amewaeleza wakazi hao kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ilishaanza mikakati ya kukabiliana na athari za mvua katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa morogoro kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Mabwawa eneo la Kidete.
Amesema kuwa ujenzi wa mabwawa hayo ya maji yatakuwa ni suluhisho la kudumu ya mafuriko katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro.
Ameongeza kuwa kwa sasa mpango huo upo katika hatua za kitalaam ikiwemo kumpata mkandarasi. ”Fedha imepatikana kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa kwa sasa tunaendelea na taratibu za kitaalam, Wizara zinazohusika hakikisheni mnakamilisha taratibu hizo ili ujenzi uanze”





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...