Na Said Mwishehe
MRADI wa mfereji wa maji uliojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)kupitia mradi wa OPEC katika vijiji vitatu vya Ngabobo, Oltepes na Tank katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha umewezesha wananchi wa vijiji hivyo kujikita katika kilimo cha umwagiliaji na hasa nyanya,vitunguu na mbogamboga.
Mradi huo wa umwagiliaji ulioibuliwa katika Vijiji hovyo vitatu vya Ngabobo, Oltepes na Tank ambapo jumla ya wakazi 4,184 wananufaika na mradi wa mfereji huo wa umwagiliaji.
Akizungumza hivi karibuni kuhusu mradi huo wa mfereji uliojengwa kupitia OPEC ,Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Meru Edwin Serumkuma amesema mfereji huo unahudumia hekta za Kilimo 1310 na zaidi ya wakulima 851 wanatumia mfereji huu katika kilimo cha nyanya, vitunguu na mboga mboga.
Pia amesema unatumika kuzalisha mazao ya chakula kama mahindi na maharage huku akifafanua pia maji ya mfereji huo hutiririka kwa mwaka mzima na bila kupungua ambayo vilevile hutumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za binadamu kama kunyweshea mifugo namajumbani.
Kuhusu utekelezaji wa mradi huo amesema uliibuliwa na wananchi wa Vijiji vya Ngabobo, Tank na Oltepeskatika kupitia mikutano maalum katika vijiji vyote uliyofanyika kati ya Januari 21,2025 mpaka Januari 21,2025.
“Mpaka sasa mradi umekamilika na unatumika.Mradi huu umegharimu Sh.401,785,714.26 hadi kukamilika kwake. Jumla ya miradi 9 kila mmoja ukiwa na thamani ya Tshs. 44,642,857.14 imetekelezwa ambapo kila Kijiji kilitekeleza miradi 3.
“Na kila mradi ulitakiwa kujenga km 0.6 hivyo miradi 9 ilitakiwa kujenga Km 5.4, lakini mradi huu una urefu wa kilometa 7.2 na pia limejengwa daraja kubwa la kuvushia wanyama na wananchi ili kupunguza uharibifu wa mfereji.
“Pia vimejengwa vigawa maji 32 katika mfereji wote. Wakati tunatekeleza mradi huu mwaka 2021/2022 Kijiji cha Ngabobo kilipata mradi wa kujenga mita 350 wakafanikiwa kujenga kilometa moja hivyo ukiunganisha mradi wa 2021/2022 jumla mradi huu utakuwa naurefu wa kilometa 8.2. Nguvu za jamii katika mradi huu ilikua ni wananchi wenyewe kujitoa kama vibarau,”amesema Serumkuma.
Kwa upande wake Diwani Kata ya Ngabobo Gabriel Kinua amesema kabla ya mradi huo kulikuwa na changamoto kubwa kwani walikuwa tunatumia mfereji ambao ulikuwa umetengenezwa na wananchi na ulikuwa haujasakafiwa wala kutengenezwa kwa namna yeyote ile
“Hivyo kabla ya mferej kujengwa tulikuwa na changamoto kubwa ya maji hasa miezi ambayo hakuna mvua,mazao yalikuwa yanakauka na watu walikuwa wanalima kwa kiwango kidogo kwasababu maji hayatoshelezi.
“Mradi huu umekuwa na matokeo makubwa kwani tumepunguza muda maji kufika mashambani maji ,haya maji saa moja na nusu inanyesha kwa wakulima wengi.Pia maji yameongezeka kwani yalikuwa yanapotea njiani kwasababu ya mchanga na udongo kufyonza maji lakini kwa sasa maji yameongezeka na hivyo wananchi wanalima kwa wingi
“Kujengwa kwa mfereji huu pia umefanya sasa mazao yameongezeka na hivyo halmashauri inapata ushuru unatokana na mazao ya mbogamboga,”amesisitiza alipokuwa akielezea faida za mradi wa mfereji huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...