Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya TECNO mobile limited imezindua uwanja wa kisasa katika eneo la Mwananyamala ambao utakaokuwa ukitumiwa na vijana na watoto kukuza vipaji vya mpira wa miguu katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

TECNO imewekeza nguvu na malengo ya kukuza tasnia ya mpira wa miguu kwa jamii ya kitanzania ikiwamo kujenga viwanja na kukuza vipaji vya vijana chini ya umri wa miaka 17 kwenye soka ikiwa ni hatua ya awali.

Akizungumza leo Januari 10,2026 wakati wa uzinduzi wa uwanja huo uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 70, Meneja wa TECNO nchini Tanzania, Dino Han, alisema kuwa hiyo ni hatua ya kwanza ila kampuni ina mipango thabiti ya kuendelea kuchangi katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kujenga viwanja vya kisasa vingi zaidi kupitia mauzo ya bidhaa zake ikiwamo simu za mkononi.

Alitoa shukrani kwa wakazi wa Mwananyamala kwa kukubaliana na jitihada zao za kuboresha kiwanja hicho ambacho kwa sasa kina muonekano wa kisasa.

“Tunawashukuru viongozi wa Serikali pamoja na wazazi wa Mwananyamala kwa kukubali kiwanja hiki kuboreshwa ili kukidhi soka la awali kwa vijana wao, Lengo letu ni kuendeleza mauzo ya bidhaa zetu ili kuboresha viwanja vingine Zaidi,”alisema.

Katika hatua nyingine ya kukuza mpira wa miguu kwa vijana, Meneja huyo alisema kupitia mpango wa Watoto wa Power Tanzania moment watoto 20 wamechaguliwa kujiunga na Academy ya Hornet ya Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo watajifunza kwa miezi mitatu, pia wazazi wao watakabidhiwa 3,000,000 kwaajili ya kukidhi mahitaji yao na kuwa motisha ili kuendeleza vipaji vyao.

“Fedha hizi zimetokana na mauzo ya simu ya mwezi Desemba, mwaka jana, kila simu iliyouzwa Sh. 10,000 ilitengwa kwaajili ya kukuza vipaji vya mpira wa miguu, ambapo ilipatikana takriban Sh. 90,000,000,” alisema meneja huyo.

Kwa upande wake Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge aliishukuru kampuni ya TECNO mobile limited kwa hatua yake ya kukuza soka nchini kwa vijana, huku akizitaka kampuni nyingine na wadau kuwekeza katika soka la vijana.

“TECNO iwe mfano kwa makampuni mengine katika jitihada za kukuza soka letu kuanzia kwa vijana, soka ni ajira na hatunabudi kutengeneza vipaji kuanzia kwa vijana wadogo. Suala la kuboresha miundombinu ya viwanja vyetu ni muhimu sana,”alisema Meya huyo.

Wakati huo huo Juma Hussein, mmoja wa wakazi wa Mwananyamala aliishukuru TECNO kwa hatua ya kuboresha kiwanja hicho akidai kuwa mtaani kuna vipaji vingi vya soka kwa vijana wadogo, ila tatizo ni kukosa viwanja vya kisasa vya kuchezea.

“Tunapokuwa na viwanja kama hivi vingi ni fursa kwa watoto wetu wenye vipaji kuviendeleza. Uwanja huu kabla ya kuboreshwa ulikuwa ni vumbi tupu, ila sasa umewekea kapeti za uzio wa kisasa, ni wajibu wetu kuutunza kwaajili ya vizazi vyetu vijavyo, alisema Hussein

Kijana Khalid Omary, ambaye pia ni mkaazi wa Mwananyamala, aliomba wadau wengine kuendelea kujitokeza katika kuibua vipaji vya soka kwa vijana wadogo. Sisi vijana wenye vipaji vya soka, mtaani tupo wengi ila wakati mwingine tunakosa mtu wa kutushika mkono kama walivyofanya TECNO, tunaomba wadau wazid kujiti kujitokeza,” alisema Omary

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...