Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi, bidii na ubunifu ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa Nusu ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/26.
Bw. Mwenda ametoa wito huo Ijumaa, Januari 9, 2026, wakati akihitimisha Mkutano wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa TRA kwa Nusu ya Mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Amesisitiza kuwa jukumu la ukusanyaji wa kodi ni la watumishi wote wa TRA na siyo maafisa kodi pekee, hivyo kila mtumishi anapaswa kutumia weledi, ubunifu na kuzingatia maadili ya kazi ili kufanikisha lengo la TRA la kukusanya Shilingi trilioni 36.066 katika Mwaka wa Fedha 2025/26.
Aidha, Kamishna Mkuu Mwenda amesema ni matarajio yake kuona TRA inakusanya kodi kwa ufanisi mkubwa na hatimaye kuliwezesha Taifa kujitegemea kupitia mapato yake ya ndani.
“Na mimi ninatamani siku moja TRA iiwezeshe nchi yetu kuweza kujitegemea,” alisema Bw. Mwenda.
Akizungumzia mikakati ya ukusanyaji wa mapato kwa Nusu ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/26, Bw. Mwenda amesema TRA imejipanga kuendelea kutumia mifumo ya kisasa ya kidijitali, akitaja mfumo wa IDRAS unaotarajiwa kuanza kutumika rasmi Februari 9, 2026.
Mikakati mingine ni pamoja na kupambana na ukwepaji wa kodi, kuzuia magendo, kudhibiti mipaka, kuendelea kujenga uwezo wa watumishi kitaaluma pamoja na kuhakikisha wanapatiwa vifaa stahiki ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Pia, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha TRA kupata watumishi wapya, huku akitoa wito kwa viongozi wa mamlaka hiyo kuhakikisha watumishi hao wanasimamiwa ipasavyo ili walete tija katika utendaji kazi wao.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, amewataka watumishi kuendelea kuboresha huduma kwa walipakodi, kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kupambana na mbinu mbalimbali za ukwepaji wa kodi.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Bw. Moshi Jonathan Kabengwe, amewapongeza wajumbe wote walioshiriki mkutano huo na kuwataka kuyatekeleza maazimio yote yaliyofikiwa ili TRA iendelee kuvuka malengo ya makusanyo.
Aidha, amewapongeza watumishi wa TRA wanaotarajiwa kustaafu ndani ya mwaka 2026, akisema wameacha alama chanya katika utendaji wao wa kazi.
Mkutano huo wa siku tano wa tathmini ya utendaji kazi wa TRA kwa Nusu ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2025/26 uliwashirikisha jumla ya washiriki 477 kutoka ofisi za TRA nchini kote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...