NA MWANDISHI WETU
WWAHITIMU  kidato cha Nne na darasa la Saba ambao wamekosa sifa za kuendelea na masomo kujitokeza kujiunga na Chuo Cha Ufundi Furahika kupata elimu ya ujuzi bure unaoendana mahitaji katika Soko la ajira.

Chuo hicho kimeweka mikakati endelevu ya kutafutia wahitimu wao wa ajira ili wasiwe mzigo wa ujuzi wao kuona hakuna anayehitaji

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kwamba wahitimu wote wanapokelewa bila ubaguzi wa aina yoyote.

"Tunaendelea na kampeni yetu ya kutoa elimu bure kwa vijana wote wa Kitanzania ambao wapo katika mazingira magumu na tunafanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutimiza ndoto za kundi hilo kupitia elimu ili wajikomboe maishani.

"Tunawapongeza wanafunzi wote waliomaliza kidato cha Nne na kufanya vizuri katika masomo yao ni jambo jema sana ila wasiishie tu hapo tunahitaji kuona akili hiyo wanaihamishia vyuoni.

" Ipo kasumba kwa baadhi wanafunzi wanafanya vizuri wakiwa Sekondari na wanapofika vyuoni wanaporomoka kiwango, sijui shida iko wapi, nawaombea kwa Mungu waendelee kufanya vizuri hadi vyuoni.

Pia amewataka wazazi, walezi wasiwaache Vijana wao nyumbani kwa kukosa ada, wawapeleke katika chuo hicho ili kupata ujuzi katika fani hoteli, umeme, udereva, ususi, bandari, Ufundi bomba na nyinginezo ambapo watasoma Bure kupitia mrado wa elimu bure na watakachogharamia na fomu na vifaa

Ameongeza kuwa dirisha liko wazi hadi Februari 28 mwaka huu, kwa hiyo yoyote anayepata taarifa hiyo hamjulishe mwenzake popote hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...