Na Nasra Ismail- Geita
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Geita Karia Magaro amewataka madiwani kusimamia Sheria kanuni na taratibu za uendeshaji wa Halmashauri ili kuhakikisha maamuzi yanayochukuliwa yanafanyika kwa hekma na busara.
Ameyasema hayo wakati alipohitishimiaha hotuba yake katika mkutano wa kawaida wa robo ya pili wa Baraza la madiwani mwaka wa fedha 2025/2026.
Bwana Magaro amewaomba madiwani kusimamia utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa pamoja na kuhimiza ushirikiano Kati ya madiwani na watumishi ili kulinda utulivu wa halmashauri hiyo.
Halmashauri imefanikiwa Kukusanya Shilingi Bilioni 6.3 ya mapato ya ndani sawa na asilimia 45.42 ya mapato yaliyotarajiwa kukusanywa kwa mwaka huku
Halmashauri hiyo iliwa imepanga kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 20.9 kutokana na mapato ya ndani, wahisani na Serikali Kuu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Silvester Kahesi amewapongeza madiwani na wataalam kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana katika vikao vya kamati hadi kufikia baraza.
" Ushirikiano hautakuja kama kuna upande utakuwa umejitenga, nitoe wito kwa madiwani na wataalam kuwa kitu kimoja ili kuleta ufanisi na kuijenga halmashauri kwa kuwa Sisi ni taswira ya Halmashauri hivyo kile tunachokifanya kika akisi matamanio ya wananchi” Amesema Mhe Kahesi.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Geita amelilekeza Baraza la haashauri ya wilaya ya hiyo kusimamia na kuimarisha Hali ya usafi katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro ambao Hali yake hairidhishi.
Akitoa maelekezo hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita katibu tawala wa wilaya hiyo Lucy Beda alisema kuwa Baraza Lina jukumu la kusimamia Hali ya usafi katika mji huo ili uendane na Hadhi yake.
"Katoro mji mkubwa unaoendelea ni vyema kama Baraza mkashirikiana kuhakikisha mji ule unakuwa safi kuendana na jina na Hadhi yake, viongozi wakubwa wanapokuja Geita ni lazima wasimame Katoro ili wasalimie wananchi ni vyema mji huo ukiwa katika Hali ya usafi" alisema Beda.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...