Na Hassan Kimweri, WAF - Manyara

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau kutoka Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) imefanya kikao kazi kwa lengo la kutathmini namna bora ya kuendeleza utoaji wa huduma bora za afya kufuatia kupungua kwa mchango wa wafadhili duiniani.

Akiongea wakati wa kikao hicho, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema kikao kimefanyika kwa wakati muafaka, hasa ikizingatiwa tayari wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya ya kuchukua jukumu la kuandaa mpango mkakati wa uendelevu wa huduma za afya nchini.

"Huduma za afya ni lazima ziendelee kutolewa kwenye maeneo yote muhimu ikiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria, Afya ya Mama na Mtoto, Magonjwa Yasiyoambukiza usafirishaji wa sampuli na ajira za wataalamu wa sekta ya afya. licha ya mabadiliko ya ufadhili wa afua za Afya duniani, kote”amesema Dkt. Magembe

Dkt. Magembe amesema, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 142 kama fedha za awali kwa ajili ya ununuzi wa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV), Kifua Kikuu, Malaria pamoja na vifaa vya uchunguzi, hatua inayolenga kuwa na uendelevu wa huduma.

Amezitaja hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuandaa mpango wa uendelevu wa huduma (Sustainability Plan), kuanzishwa kwa Bima ya Afya kwa wote, kutoa huduma jumuishi (Integration of Health Services), kutenga vyanzo mahususi vya fedha za ndani kugharamia huduma za afya na kuimarisha mifumo ya kidijitali na huduma za afya ngazi ya msingi.

Pia amewapongeza wadau wa maendeleo, hususan EGPAF, kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha mifumo ya afya, akitolea mfano wa kazi iliyofanyika katika mkoa wa Manyara ambapo ziara ya vituo vya afya imeonesha mchango mkubwa wa wadau katika kuhakikisha huduma bora na endelevu zinawafikia wananchi.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...