WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) anatarajiwa kuzindua Miradi mikubwa ya kuendeleza Utalii Kusini siku ya jumatano tarehe 11 Februari, 2026.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Februari 9, 2026 amekagua maandalizi ya uzinduzi wa miradi ya kuendeleza utalii kusini.

Miradi hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hapo kesho imejengwa katika hifadhi za Taifa za Julius Nyerere, Mikumi, Ruaha pamoja na Msitu wa Asili Kilombero na imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 100.

Uzinduzi wa Miradi hiyo mikubwa iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa dhumuni la kukuza na kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania utafanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

Tayari Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasilia na Utalii Dkt. Hassan Abbas ameshakagua maandalizi ya uzinduzi huo na kusema kuwa maandalizi yamekamilika ambapo miradi hiyo imejengwa kwa kiwango kinachohitajika na inatarajiwa kuwa kichocheo cha kuongeza watalii wanaotembelea hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...