Wanawake watumishi wa Mamlaka  Hifadhi ya Ngorongoro katika muendelezo wa  kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, wamedhihirisha kwamba mchawi wa mwanamke si mwanamke  kwa kutembelea  shule ya Sekondari ya wasichana Ngorongoro na kuwapa tabasamu la  msaada wa vifaa mbalimbali

Akiongea kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Afisa Uhifadhi Mkuu Sarah Lushu ameeleza kuwa vitu ambavyo Mamlaka vinajumuisha vyakula, Sabuni, vifaa vya kujifunzia, taulo la kike, Vyombo vya kuogea, kupikia na kufulia na mahitaji mbalimbali mahususi kwa wanafunzi wanawake ilo kuwaongezea tabasabu na kuonyesha nguvu ya mwanamke katika Jamii.

"Msaada huu ni sehemu ya jitihada za Shirika kupitia kamishna wa Uhifadhi kuimarisha uhusiano na jamii iliyopo ndani ya Hifadhi na kuhakikisha kuwa wanafunzi hasa wa kike wanapata mahitaji muhimu ya kuwapa utulivu wa kusoma na kupata ufaulu mzuri" alifafanua PCO Sarah.

Msaada huu unadhihirisha wazi kuwa wanawake ni watu wa kusaidiana na mchawi wa mwanamke sio Mwanamke. 






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...