Watu kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Mlima “S”, kijiji cha Lumango, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya ZL Super Safari lililokuwa likitoka Ifakara kuelekea Morogoro, pamoja na lori lililokuwa limebeba kokoto.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu bajaji iliyokuwa mbele yake, hali iliyosababisha kugongana na basi hilo.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ili kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...