
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imefanikiwa kukamata dawa za kuelevya aina ya mirungi kilo 106.25 katika wilaya ya Longido mkoani Arusha zikiwa zinasafirishwa kwa gari aina ya Toyota Wish yenye namba ya usajili T 889 DPG.
Akizungumza leo Aprili 14,202 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema katika tukio hilo Diwani wa Kata Kimokouwa Solomon Koholo (38) na Lekaneti Kukuu (38) wanashikiliwa kutokana na tuhuma hizo.
Akifafanua zaidi kutokana na tukio hilo amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu maarufu kutumika kwa namna moja au nyingine katika biashara ya dawa za kulevya ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kuwa mamlaka hiyo haitasita kumchukulia hatua yeyote yule hata awe maarufu kiasi gani.
Mbali na tukio hilo pia amesema katika Mkoa waKilimanjaro, eneo la Himo na Same, zimekatwa kilo 68.3 za mirungi zilizowahusisha watuhumiwa Amin Mazua (58) maarufu kwa jina la Mbaruku na Wilbard Mchau (50).
Akieleza zaidi kuhusu operesheni za mamlaka hiyo amesema sambamba na Sambamba na udhibiti wa mirungi, aina nyingine ya dawa za kulevya zilikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...