Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi Mabalozi wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbalimbali kutanguliza mbele maslahi ya Taifa ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.
Makamu wa Rais amesema hayo, wakati akizungumza na Mabalozi wateule wanaokwenda kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mataifa mbalimbali, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma kwa lengo la kuwaaga mabalozi hao.
Amewaasa kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo nchini na kuwashawishi wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza nchini.
Aidha, amewataka Mabalozi hao kusimamia maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki anachojenga uchumi wa nchi na kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
Makamu wa Rais, amewaagiza Mabalozi hao kuhakikisha wanasimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na miongozo mbalimbali kutoka Serikalini.
Makamu wa Rais amewapongeza Mabalozi hao kwa kuaminiwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwenda kuiwakilisha nchi katika Mataifa mbalimbali na kuwasihi kutumia vema imani hiyo waliyopewa.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mabalozi, Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Maulidah Hassan amemshukuru Makamu wa Rais kwa muongozo, maelekezo na ushauri aliyotoa na kuahidi kufanya kazi kwa bidii.
Mabalozi hao wateule waliofika kwaajili ya kuaga kabla ya kwenda kwenye vituo vyao ni pamoja na Mhe. Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said (Saudi Arabia) Mhe. Balozi Cyprian Luhemeja (Zambia), Mhe. Balozi Maulidah Hassan (Oman), Mhe. Balozi Salim Othman Hamad (Comoro), Mhe. Balozi Swahiba Mndeme (Sweden), Mhe. Balozi Noel Kaganda (Korea) na Mhe. Balozi Musa Haji Ali, Naibu Mwakilishi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...