Arusha
SERIKALI  imesema haina mpango wa kusimamisha ama kuzuia shughuli za uwindaji wa kitalii na badala yake inaendelea kuandaa na kuboresha sera,sharia na miongozo itakayohakikisha uwindaji wa kitalii unafanyika kwa kuzingatia uhifadhi wa wanyamapori, kukuza mapato ya Taifa na kuchochea maendeleo ya jamii.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi kati ya chama cha wamiliki wa kampuni za uwindaji Tanzania, katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuenzi sekta ya wanyamapori kwakuwa ni rasilimali ya kipekee yenye mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa, uhifadhi wa mazingira na ustawi wa jamii na hivyo haina mpango wa kuisimamisha bali kuiendeleza.

Ameongeza kuwa ni matarajio ya mkutano huo kuwa utabainisha mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya uwindaji wa kitalii ili kujenga ustawi na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la uwindaji wa kitalii kimataifa.

Amewataka wadau hao wa uwindaji wa kitalii kuilinda sekta hiyo kwa kuzingatia maadili na kuendeleza uhifadhi na kupmabana na ujangili, kutokukwepa kodi, kulipa kodi na stahiki za jumuiya au wananchi zinazozunguka maeneo ya ya uwindaji.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Alexander Lobora amesema mikutano ya aina hii imekuwa na tija kwa Serikali na wadau wa tasnia ya uwindaji wa kitalii katika kutafuta suluhu ya changamoto kubwa zinazoikabili tasnia hii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji Tanzania (TAHOA); Bw. Michel Mantheakis, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwa tasnia hiyo na kuongeza kuwa Chama hicho kitaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia sheria na taratibu kwa kuwa kushuka ama kusimama kwa uwindaji wa kitalii ni kukosekana ama kushusha mapato ya serikali lakini pia kudhorota kwa uhifadhi na hivyo kutokomea kwa uwindaji wa kitalii.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...