NA Mwandishi Wetu

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es salaam linaendelea kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan la kuhakikisha wanafunzi wote wa darasa la 6 na 7 wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi kwa mkupuo (Double Cohort) 2027 wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028.

Katika kuhakikisha agizo hilo linafanikiwa, Halmashuri hiyo imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kujenga shule kwa mtindo wa ghorofa ambapo nyingine zimekamilika na nyingine zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2025/26,Halmashuri ya Jiji la Dar es salaam imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 19 katika sekta ya elimu Sekondari kuhakikisha adhima hiyo inafanikiwa.

Jumla ya shule za ghorofa 9 mpaka sasa zimejengwa zikiwemo mpya na zile zilizoboreshwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa.

Shule hizo ni pamoja na shule mpya ya  Kitunda Relini iliyojengwa kwa gharama za Shilingi bilioni 4.2,Kipunguni B (bilioni 2.1),Bonyokwa(bilioni 2),Ukonga (bilioni 2.2),Minazi Mirefu (bilioni 2.3),Mnazi Mmoja (kumalizia ujenzi bilioni 1.8), Liwiti(bilioni 2.1) pamoja na kumalizia ujenzi Sekondari Kimanga(milioni 998).

Mbali na ujenzi huo, baadhi ya shule hizo zimefungiwa mfumo wa "lift" kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam inatarajia kuwa ifikapo muhula wa 2027/28 iwe imekamilisha mahitaji ya wanafunzi wote wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza kwa muhula huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...