Na; Mwandishi Wetu

Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Mikutano ya Baraza la Wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kujadili utekelezaji wa majukumu, kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na weledi.

Amesema ili kuendelea kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu, ni muhimu kudumisha utamaduni wa kufanya kazi kwa umoja, bidii na weledi. Tunapaswa kujipambanua kwa utendaji wa hali ya juu unaoendana na hadhi ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika nchi.

Mhe. Masauni ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais uliofanyika Dodoma, Aprili 15, 2026 akieleza kuwa Ofisi imeendelea kufanya vizuri katika kudumisha Muungano, hususan kupitia utoaji wa elimu kwa umma kwa makundi mbalimbali.

“Kwa upande wa usimamizi wa mazingira, Ofisi imefanikiwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191, hususan kwa kuimarisha vifungu vinavyohusu mabadiliko ya tabianchi na kuanzisha Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC).

Aidha, ni muhimu kuendelea kuimarisha uwezo wa kitaalam na kitaasisi, upatikanaji wa rasilimali na kuongeza jitihada za uhamasishaji wa rasilimali fedha, ikiwemo kupitia maandalizi bora ya miradi ya uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alisema lake kuu tangu kuanzishwa kwake baraza hilo lilikuwa kuimarisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kupanga, kutekeleza na kutathmini mipangokazi, pamoja na kuboresha uhusiano kati ya Menejimenti na watumishi.

“Madhumuni ya Mkutano huu ni kuwashirikisha wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kupata Taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Ofisi.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu waRais uliofanyika Dodoma, Aprili 15, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais uliofanyikaDodoma, Aprili 15, 2026. Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu waRais, Mhe. Reuben Kwagilwa, wa Kwanza kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi na wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Mitawi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akiwa na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Raisuliofanyika Dodoma, Aprili 15, 2026.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...