Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara (SADR), Mhe. Brahim Ghali. Katika mazungumzo hayo, aliwasilisha salaam za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 9 Aprili 2026 katika makazi rasmi ya Mhe. Ghali, Kambi ya Ausserd, Tindouf, Algeria. Balozi Migiro alisisitiza kuwa msimamo wa Tanzania na CCM wa kuunga mkono haki ya watu wa Saharawi kujitawala ni wa muda mrefu. Alieleza kuwa msingi wake uliwekwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wake, Mhe. Ghali alimshukuru Rais Dkt. Samia kwa salaam na kwa kutuma uwakilishi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya SADR yaliyofanyika tarehe 8 Aprili 2026 katika Kambi ya Ausserd. Pia aliomba salamu zake zifikishwe kwa Rais, CCM na Watanzania.

Aliongeza kuwa watu wa Saharawi wanathamini mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhamasisha mshikamano wa Afrika na dunia. Alisema mshikamano huo umeendelea kuimarisha harakati za SADR, chini ya uongozi wa Chama cha Polisario, katika kudai haki ya kujitawala.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...