Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndugu Wazo Mwang’onda, ameipongeza TARURA wilaya ya Ruangwa kwa usimamizi mzuri wa mradi wa barabara ya Mwilala yenye urefu wa kilomita 0.59 kwa kiwango cha lami.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo, Mwang’onda alisema ameridhishwa na ubora wa ujenzi huo ambao umejumuisha mitaro na kusimamiwa kwa viwango bora. 

Meneja wa TARURA wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Nalupi alisema mradi huo uliojengwa na M/S JATL TECH & CONSTRUCTION COMPANY LIMITED umegharimu shilingi 513,320,500.00.

Lengo la mradi ni kuboresha usafirishaji kwa wakazi wa vijiji vya Likangara, Dodoma, Nachingwea na Mchanganindani. Mhandisi Nalupi aliongeza kuwa barabara ya lami imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

Wananchi wa Ruangwa wamesema barabara hiyo imeleta faraja, kwani sasa wanaweza kufanya biashara hata nyakati za usiku kutokana na kuwepo kwa taa za barabarani. 








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...