WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikifungua dirisha kwa makada wake kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo, mwitikio umekuwa mkubwa huku makada kujitokeza kushiriki mchakato huo.
Makada hao wamefika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam, ambako wamekabidhiwa fomu hizo na Ofisa wa Chama kutoka Idara ya Organaizesheni, Raymond Mosi.
Miongoni mwa waliojitokeza ni kada kijana, Julias Mtatiro, ambaye ujio wake katika kinyang’anyiro hicho unaakisi kuongezeka kwa ushiriki wa vijana katika nafasi za juu za uongozi wa kikanda.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mtatiro amesema uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo unatokana na dhamira ya kutumia nguvu, maarifa na mtazamo wa kizazi kipya katika kulisukuma mbele taifa ndani ya Bunge la Afrika Mashariki.
Mtatiro ameeleza kuwa vijana wana mchango mkubwa katika kuleta mageuzi chanya, ubunifu wa sera na kuimarisha ushirikiano wa kikanda unaolenga maendeleo jumuishi.
Aidha, amesisitiza anajitosa si tu kama haki yake ya msingi, bali kama wajibu wa kizazi cha vijana kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya kimkakati yanayogusa mustakabali wa taifa na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...