Na Mwandishi Wetu
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikifungua dirisha kwa makada wake kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo,Kada wa Chama
hicho ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga amechukua fomu kuwania nafasi hiyo.
Mtatiro ambaye ni miongoni mwa makada vijana na wasomi katika Taifa la Tanzania amechukua fomu hiyo ya kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo Aprili 18,2026 katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, zilizopo Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Amekabidhiwa na fomu hiyo na Ofisa wa Chama Idara ya Organaizesheni, Raymond Mosi.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu Mtatiro amesema ameamua kujitosa katika kinyang'anyiro hicho kutumia haki yake ya msingi katika kuliwakilisha taifa katika Bunge la Afrika Mashariki kwa maslahi mapana ya taifa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...