Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Uingizaji na Usambazaji wa mafuta Jamii ya Petrol nchini ya 'MOIL Energies' imesema imefurahishwa kwa kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ulipaji kodi ya nishati hiyo kabla ya kuyatoa vituoni na kwenda sokoni (BIL)kwa kiasi kikubwa umesaidia kudhibiti 'ujanja ujanja' uliokuwepo hapo awali

Akizungumza Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo nchini, Dkt Sajad Habib Rai amesema wao kama Kampuni ya kwanza nchini kutoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa mfumo huo kwa EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na baadae kuanzishwa rasmi na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), wanajivunia kuona umetekelezwa kwa kuwa dhamira yao ilikuwa kuona huduma ya usambazaji wa mafuta nchini na nje ya nchi unaleta tija kwa Taifa.

"Tumefurahi kuona TRA wameusimamia kikamilifu mfumo huu kwa kuwa unazuia ukwepaji kodi ambao hapo awali ulikuwa ukifanywa na wafanyabiashara, hivi sasa TRA inapata kodi yake mapema kabla ya kuyaingiza mafuta sokoni" amesema Dk Sajad ambaye pia ni Meneja MKAZI wa 'Mansoor Industry Limited'

Hivi karibuni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza rasmi kuanza kutumika kwa mfumo huo ambao kwa kiasi kikubwa unalezwa kuleta tija kwa Serikali kwa kuwa umesaidia kudhibiti upotevu wa mapato unaotakana na Kodi za uingizaji wa mafuta hayo nchini.

Kupitia mfumo huo mpya na wa kisasa, kila mwagizaji au muingizaji wa mafuta atalazimika kutaja kiasi cha mafuta alichokiingiza nchini ambapo kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) watayataweka vinasaba kama alama ya kila mwagizaji kwa lengo la kuwatambua wahusika wote na kiasi alichoagiza ili kuwakadiria viwango vya Kodi wanavyopaswa kulipa.

"Nawapongeza TRA kwa kuona tija na umuhimu wa kuutumia mfumo huu, sisi kama wafanyabiashara tunaozingatia taratibu halali za uingizaji na Usambazaji wa mafuta tunaiona kuwa hatua hii ni kubwa na inayostahili kupongezwa kwa kuwa italeletea manufaa Taifa" ameongeza Dkt Sajad

Utaratibu huo wa kikodi unawataka wamiliki wa mafuta hayo kuyalipia kodi kabla ya kuyaingiza sokoni ili yanapoingizwa sokoni yanaendelea na taratibu za uuzwaji hali ambayo inarahisisha usambazaji na kuwafikishia wateja huduma ya mafuta kwa wakati sambamba na kudhibiti kubaki nchini mafuta ambayo kimsingi yanapaswa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Aidha akizungumza wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika bohari za kuhifadhia mafuta zilizopo Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda pamoja na mambo mengine alisema lengo la TRA kuweka utaratibu huo ni kuwezesha biashara kufanyika kwa urahisi na kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali huku akitoa wito kwa wafanyabiashara watakaokutana na changamoto zozote kuwasiliana na TRA.

Pamoja na mambo mengine pia Kamishina Mwenda alisema Mamlaka hiyo pia umeweka utaratibu wa kufanya kazi kwa Saa 24 ili kuharakisha utolewaji wa huduma kwa walipakodi ambao ni waingizaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta hayo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...