Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amezindua rasmi huduma ya umeme katika vitongoji 15 vya jimbo hilo kupitia mpango wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Uzinduzi huo umefanyika Aprili 10, 2026 katika Kitongoji cha Mtonya na Mandepwende, kilichopo Kata ya Ruinga, ambapo Mheshimiwa Homera amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya umeme.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Homera alieleza kuwa kuwashwa kwa umeme katika vitongoji hivyo 15 ni mwanzo wa mpango mpana zaidi, ambapo serikali kwa kushirikiana na REA imejipanga kuhakikisha kila mwezi vitongoji vipya vinaunganishwa na huduma ya umeme katika jimbo hilo.
Amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata umeme bila kujali hali ya makazi yao, akieleza kuwa hata nyumba za nyasi au zilizojengwa katika mazingira tofauti zinapaswa kufikiwa na huduma hiyo muhimu.
Kwa upande wake, Deo Nangu, aliyewakilisha Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Hassan Said, amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6.
Mradi huo unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme, kuchochea shughuli za kiuchumi, na kuboresha maisha ya wananchi wa Namtumbo kwa ujumla.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...