Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imesema mkakati wake ni kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku pia ikisisitiza umuhimu wa elimu ya mara kwa mara kwa watumiaji ili wawe na uelewa namna bora ya kutumia nishati safi ya kupikia
Hivyo katika kufanikisha mkakati huo Oryx Gas imesema imeamua kuanzisha maduka maalum yatakayotumika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi kwa kusogeza huduma hiyo karibu lakini wakati huo huo maduka hayo yatatumika kutoa elimu ya matumizi bora na salama ya nishati safi.
Akizungumza leo Aprili 30,2026 wakati wa ufunguzi wa duka maalum la kuuza mitungi ya Gesi ya Oryx lililopo eneo la Banana jijini Dar es Salaam Menaja Masoko na Mauzo Shaban Fundi amesema wanatambua juhudi za serikali katika kuhimiza nishati safi.
“Sisi Oryx Gas ni vinara wa nishati safi ya kupikia hivyo tumeunganisha nguvu zetu kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia yanafika kwa wananchi wote.Tunatambua namna gani Serikali inatamani ifikapo mwaka 2030 basi asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia
“Kwahiyo ufunguzi wa maduka haya maalum ni muendelezo wa muunganiko wetu kuunga mkono juhudi za Serikali na wananchi kwa ujumla kwamba nishati safi sio anasa bali ni lazıma kwamba watu wapate nishati safi ya kupikia na sisi kama Oryx tumeendelea kuboresha miundombinu ya kuhifadhi ,kupokea pamoja na usambazaji lengo ni kuona huduma inafika kwa jamii.”
Kuhusu elimu ya namna bora ya kutumia nishati safi ya kupikia amesema ni jambo la msingi wananchi kujengewa uelewa kuhusu matumizi ya nishati hiyo kwani usipojua namna ya kuitumia vizuri unaweza kuona ni gharama au inakwisha mapema kumbe anayetumia hajui jinsi ya kutumia hasa kufungua mtungi au jinsi ya kuufunga.
“Kwahiyo wananchi wakifika katika maduka yetu watapata elimu ya namna gani wanaweza kutumia nishati safi ya kupikia mitingi yetu.Mbali ya kupata elimu hiyo Oryx Gas tumekuja na utaratibu wa kupeleka huduma kwa wananchi kwani ukishanunua mtu hutaubeba bali utaacha namba ya simu na sisi tutakuletea mpaka ulipo kwa gharama zetu.
“Hivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata nishati safi kwa wakati tunaendelea na kufunga maduka haya maalum ambako kwa nchi nzima yapo 1000 na tunaendelea kufungua mengine likiwemo hili la Banana kwa NASSCO na wiki iliyopita tumefungua duka Masenze.”
Kwa upande wake Tarik Nassoro ambaye ni Mkurugenzi wa NASSCO ambayo Wakala wa Oryx Gas amesema kwa kushirikiana na Oryx wamefungua maduka katika maeneo mengi wilayani Ilala huku akiwaomba Watanzania kuendelea kutumia gesi ya oryx na waache kutumia nishati ambazo zinachafua mazingira .
Wakati huo huo Baba Lishe Dickson Kuga na Mama Lishe Beatrice Shayo wametoa rai kwa mama na baba lishe nchini kutumia nishati safi ya kupikia katika kuandaa chakula kwani nishati safi inaokoa muda lakini pia haina madhara kiafya kama wakitumia kuni na mkaa.




.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...