Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema vijana ndio nguzo kuu ya uendeshaji wa Serikali ya awamu ya sita, akisisitiza kuwa mustakabali wa taifa uko mikononi mwao kutokana na idadi yao kubwa nchini.

Akizungumza katika Kongamano la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Tunguu, Zanzibar, Rais Samia alisema takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha wazi kuwa vijana ndio kundi kubwa la Watanzania, hivyo wanapaswa kupewa nafasi pana zaidi katika maamuzi ya maendeleo ya taifa.

Amefafanua kuwa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuboresha mazingira ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika uongozi na kujenga taifa lenye ushindani.

“Serikali hii inaendeshwa na vijana. Sisi tuliopo juu kazi yetu ni kutoa mwelekeo, kusimamia sera na kurekebisha mifumo ya kisheria pale inapohitajika,” alisema Rais Samia.

Aidha, amebainisha kuwa muundo wa sasa wa Serikali unaonesha dhamira hiyo, ambapo idadi kubwa ya mawaziri na manaibu mawaziri ni vijana. Aliongeza kuwa hata katika vikao vya Baraza la Mawaziri, zaidi ya robo tatu ya wajumbe waliohudhuria walikuwa chini ya umri wa miaka 50.

Rais Samia amesisitiza kuwa hatua hiyo si ya bahati mbaya, bali ni utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa pamoja na maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambayo inaelekeza kuwekeza nguvu zaidi kwa vijana.

Kwa upande mwingine, aliwataka vijana kote nchini kutumia fursa wanazopewa kwa uwajibikaji, nidhamu na uzalendo, ili kuhakikisha wanachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ustawi wa jamii.












Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...