TAMASHA la Utalii la Same festival linalofanyika kila mwaka wilayani Same mkoani Kilimanjaro limetajwa kuwa chanzo cha kuchochea idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mhifadhi wa hifadhi hiyo, Kamishna Emmanuel Sisiya katika uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika wilayani Same, ambapo alisema kuwa hapo nyuma wageni waliokuwa wakitembelea hifadhi hiyo walikuwa wachache.

Alisema kuwa, tamasha hilo limekuwa chachu na hamasa kubwa ya kutangaza hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambapo kabla ya kuanzishwa tamasha hilo idadi ya wageni waliokuwa wakitembelea hifadhi walikuwa wachache lakini kwa sasa wameongezeka ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita walipokea wageni 7700 na katika wageni hao 4000 ni Watanzania.

"Wageni wengi wamechangiwa na hamasa kubwa inayofanywa kupitia tamasha hili la Same Utalii festival na kila anayekuja anakiri kuwa yeye ameifahamu Mkomazi kupitia matamasha mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika kuitangaza Mkomazi hivyo nirudishe pongezi kwa Mkuu wa wilaya Kasilda Mgeni kwa kuanzisha tamasha hili " Alisema Kumishna Sisiya.

Aliongeza kuwa, kwa sasa hifadhi hiyo ina fursa ya uwekezaji ambapo yapo maeneo kwa wageni kuja kuwekeza maeneo ya malazi na hoteli kwani wageni wengi wanaofika Same hudai eneo la malazi hayatoshi.

Alisema kuwa, ndani ya hifadhi maeneo ya malazi yaliyopo hayatoshi hivyo sasa ni fursa kwa Watanzania kuwekeza ndani ya hifadhi hiyo.

"Hifadhi ya Mkomazi katika Kanda ya Kaskazini ni ya pili ambapo ukifika utaweza kuwaona wale wanyama wakubwa watano tofauti na hapo katika Kanda ya Kaskazini utaweza kuwaona Serengeti na Ngorongoro lakini kwa urahisi na kwa ukaribu ukitaka kumwona faru mweusi utamwona ndani ya hifadhi ya Mkomazi" alisema.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...