Sekta ya Sheria siyo ya huduma ila miundombinu laini kufikia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Rwezimula alisema kuwa Dira ya Taifa 2050 imezingatia na kujikita kwenye Sekta ya Sheria ambapo Sekta ya Sheria ni msingi wa kufikia Dira 2050, mazingira ya sheria yamezingatiwa na kupewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa sheria zinatumika kama miundombinu katika kufanikisha utekelezaji wa Dira hiyo ili kuwaletea wananchi maendeleo.

“Kumekuwa na mtazamo kuwa Sekta ya Sheria inahusika na utoaji wa huduma pekee bali ukweli ni kwamba Sekta hii ni miundombinu muhimu ya kufanikisha utekelezaji wa majukumu na hivyo taifa kujiletea maendeleo,” amesema Dkt. Rwezimula.

Pia, ameipongeza OWMS kwa kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali ndani na nje ya nchi kwa ufanisi na weledi na amewakumbusha kuwa lengo la kuwa na Baraza hilo mahali pa kazi ni kuwawezesha wafanyakazi kushauri menejimenti na kushirikiana katika kutekeleza majukumu.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi alisema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 2025 hadi Aprili, 2026 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendesha jumla ya mashauri 10,400 ya madai ambapo kati ya mashauri hayo, mashauri 642 yalikamilika na OWMS imeshinda mashauri 563 sawa na asilimia 88%.

“Ushindi huu wa uendeshaji wa mashauri kwa niaba ya Serikali na taasisi zake ni dhahiri kuwa OWMS imeitendea haki Serikali,” amesema Dkt. Possi.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo amesema kuwa OWMS inawashirikisha wafanyakazi katika majadiliano ya pamoja ya utekelezaji wa majukumu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Rwezimula alizindua Mkakati wa Mawasiliano wa OWMS (OSG Communication Strategy) ambapo Mkakati huo utaiwezesha Ofisi hiyo kuwa na mwongozo wa kufanya mawasiliano ya kimkakati baina ya Ofisi hiyo, wadau na wananchi, kuchambua na kuainisha njia za mawasiliano, ukusanyaji wa mrejesho na namna ya kufanyia kazi ili OWMS iweze kutumia lugha nyepesi na rahisi kuwasiliana na wadau na wananchi kwa ujumla.

Kikao hicho cha Baraza kimeshirikisha wajumbe na wawakilishi wa OWMS kutoka mikoa 18 ya Ofisi hiyo ambapo inatekeleza majukumu yake.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa Mkutano wa Baraza la Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa Mkutano wa Baraza la Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula (aliyesimama katikati) akiwaongoza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuimba wimbo wa mshikamano daima wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula (aliyesimama katikati) akikata utepe kuzindua Mkakati wa Mawasiliano wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OSG Communication Strategy) baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma. Anayeshuhudia kushoto kwake ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula (aliyesimama katikati) na viongozi wengine wakionesha Mkakati wa Mawasiliano wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kuuzindua wakati wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula (aliyesimama kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi za mikoa za Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufungua mkutano wa Barza hilo uliofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufungua mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...