Mwandishi wetu.
MWAKILISHI wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mussa Azzan Zungu, Bi.Hellen Madanganya, amewapongeza walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya awamu zilizopita na kuwatia moyo kuwa kutokana na umakini alionao Spika Mussa Azzan Zungu, changamoto zote zilizotajwa kwenye mahafari hayo anaamini atazifanyika kazi huku akiwataka wanafunzi hao kuiga mifano na kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani ijayo .
Katibu Madanganya aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafari ya 26 ya Kidato cha sita yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule hiyo ambapo wanafunzi waliyofanya mahafari hayo walikuwa ni 314, wasichana 145 na wavulana 169.
Alisema kuwa amepokea taarifa za changamoto zilizosomwa kwenye risala ya Mkuu wa Shule hiyo Juma Boniface Orenda na kusema kuwa yeye akiwa Mwakilishi wa Spika atafikisha ujumbe huo na anaamini utafanyiwa kazi na kusema kuwa yeye hataweza kujibu risala hiyo badala yake ataifikisha kwa Spika jinsi ilivyo.
“Mimi nipo kwa Itifaki ya Spika kwa maana ya kwamba ni mwakilishi, lakini ninapenda kuwahakikishia kwamba Spika wetu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala ni mtu makini sana ambaye ninaamini yote haya ataenda kuyashughulikia kwa haraka zaidi,” alisema Kiongozi huyo.
Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Kibasila Dkt. Juma Orenda, alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa waliyoyapata hasa kwenye ufaulu mkubwa wa wanafunzi waliopita lakini wamekuwa wakipokea maelekezo mbalimbali ya kiserikali na kuyafanyia kazi likiwemo suala kubwa la kuzitaka shule zote kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula mashuleni na kusema kuwa suala hilo wamelikamilisha kwa asilimia 100 na kwamba watoto wanapata chakula na kwa wakati.
“Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa Ofisi ya Spika wa Bunge na Mbunge Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu kwa kutambua mwaliko wetu na kututumia mwakilishi wake Bi. Madanganya, hili ni jambo kubwa sana na la kufurahisha,” lakini pia kupitia kwa kiongozi huyu nipende kusema kuwa tunazo changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni pamoja na ile ya kutokuwa na gari maalumu inayoweza kutusaidia pindi tu inapotokea changamoto za kiafya,” alisema.
Dkt. Orenda, alisema pia changamoto nyingine ambayo shule hiyo imekuwa ikikabiliana nayo ni pamoja na kutokuwa na Sehemu ya wanafunzi kulia chakula kwa wakati na kwa pamoja (Cantiini), kutokuwa na dhamani za kutosha kama meza na vitu.
“Lakini pia Mhe. Tunayochangamoto nyingine ambayo ni kwa watu wenye ulemavu ambao pia wamekuwa na changamoto ya kutokuwa na fimbo nyeupe, komputa mpakato na vitendea kazi vingine,” alisema.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...