Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Neema Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa viongozi na wadau wa Afrika kuweka kipaumbele katika ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili wa kidijitali.
Akizungumza jijini Nairobi, Kenya Mei 12, 2026, katika Mkutano wa Wenza wa Mawaziri wakuu wa nchi za Afrika, uliofanyika Pembezoni mwa Mkutano wa “Africa-Forward Summit” ukilenga kujenga mazingira salama ya kidijitali kwa watoto wa Afrika katika ulimwengu unaoendeshwa na Akili Unde (AI). Bi.Nchemba alisisitiza kuwa mustakabali wa bara la Afrika hautategemea tu vigezo vya kiuchumi, bali uwezo wa watoto kujifunza na kuvumbua katika nafasi ya kidijitali bila hofu ya unyanyasaji.
Katika hotuba yake, alibainisha kuwa ingawa teknolojia ya Akili Bandia (AI) inatoa fursa kubwa katika sekta za elimu, afya, na ujasiriamali, imeleta pia hatari mpya na halisi. Alitaja changamoto kama vile uonevu mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia unaochochewa na AI, na ulaghai kama vitisho vinavyovuruga utu na maendeleo ya watoto barani Afrika.
Ameeleza hatua zilizopigwa na Tanzania, ikiwemo kufanya marekebisho ya Sheria ya Mtoto (Sura ya 13) na kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Aidha, alikumbusha Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Watoto Mtandaoni iliyoanzishwa Februari 2024 na kuundwa kamati maalum ya wadau mbalimbali ili kuhakikisha mazingira salama kwa watoto.
Mkutano huo, uliandaliwa na Kuongozwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mama Rachel Ruto ambapo ulihitimishwa kwa wito wa dharura wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na sheria madhubuti.














Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...