Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewasha moto wa kampeni katika kata za Migoli na Kihorogota, kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Ismani utakaofanyika tarehe 1 Juni, 2026.
Akizungumza na makundi mbalimbali ya wanawake na wananchi kwa ujumla, Ndg. Chatanda amebainisha kuwa CCM imeonyesha imani kubwa kwa kuweka mgombea mwanamke Ndg. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda na sasa ni jukumu la wanawake wote kuungana na kushirikiana ili kupata ushindi.
Pia amepongeza ushirikiano mkubwa na uungwaji mkono kutoka kwa wanaume wa Ismani ambao wameonyesha nia ya dhati ya kumlinda na kumsaidia mgombea wetu ashinde.
Aidha, amewakumbusha kuwa Serikali imara ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ipo madarakani na inafanya kazi kubwa. Uchaguzi huu mdogo ni kwa ajili ya kupata mwakilishi bora atakayeenda kuendeleza mazungumzo ya kimaendeleo ya Ismani bungeni.















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...