CHANGAMOTO ya afya ya akili imetajwa kuwa miongoni mwa matatizo makubwa yanayowakabili walinda amani wanaopelekwa katika misheni za kimataifa, wakiwemo kutoka Tanzania.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang’arealisema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi rasmi wa programu mbili za kimataifa za mafunzo zilizolenga kuimarisha huduma za kitabibu na msaada wa kisaikolojia kwa walinda amani wanaofanya kazi katika mazingira yenye changamoto kubwa za kiusalama duniani.
Kozi hizo maalumu zinazojikita katika msaada wa kisaikolojia na uimarishaji wa uwezo wa kitabibu, zimewakutanisha wanajeshi, wataalamu wa afya na wakufunzi kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo Canada, Rwanda, Cameroon, Indonesia, Urusi, Ujerumani na Marekani, hatua inayoonesha ushirikiano wa kimataifa katika juhudi hizo.
Brig. Gen. Itang’are alisema mtaala huo umeandaliwa mahsusi kuongeza uwezo wa walinda amani kutambua na kushughulikia changamoto kubwa za afya ya akili na matibabu wanazokutana nazo katika maeneo ya operesheni za mbele.
“Tumegundua kupitia uzoefu wa vikosi vya hivi karibuni kuwa kuna uhitaji mkubwa wa mafunzo ya aina hii kwa sababu walinda amani wanafanya kazi katika mazingira yenye msongo mkubwa unaoathiri afya ya akili na ustawi wa kijamii,” alisema.
“Ikiwa huna watumishi wenye afya njema, inakuwa vigumu kufikia ufanisi wa kiutendaji. Ndiyo maana mpango huu ni muhimu.”
Kamanda huyo alisema tathmini za hivi karibuni zilizofanywa katika operesheni za ulinzi wa amani zimebaini mapungufu makubwa katika huduma za msaada wa kisaikolojia na maandalizi ya kitabibu, hali iliyolazimisha kituo hicho kupanua kwa haraka programu zake maalumu za mafunzo.
Sehemu ya mafunzo ya kitabibu itatumia mfumo wa mafunzo kwa wakufunzi (training-of-trainers) ili kuimarisha mifumo ya afya kwa muda mrefu na kuongeza utayari wa kiutendaji kwa wanajeshi kabla na wakati wa misheni za kimataifa.
Wachambuzi walisema ushiriki wa wataalamu kutoka mataifa mbalimbali unaonesha kuongezeka kwa mwafaka wa kimataifa kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa pande nyingi katika kulinda rasilimali watu inayobeba shughuli za ulinzi wa amani duniani.
Dkt. Annie Swai, mkufunzi mkuu wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia katika TPTC, alisema afya ya akili bado ni moja ya sekta zisizoeleweka vizuri katika huduma za afya licha ya athari zake kubwa katika mazingira ya kazi ya kijeshi.
Alionya kuwa matatizo ya kisaikolojia yasipotibiwa huendelea kuwa mabaya zaidi kadri muda unavyokwenda, hali inayopunguza uwezo wa utendaji kazi, kudhoofisha majukumu ya kijamii na kuyumbisha mshikamano wa taasisi.
Dkt. Swai alisema mazingira yenye presha kubwa katika misheni za ulinzi wa amani huwafanya wengi kubeba kimya kimya msongo mkali wa mawazo, wasiwasi na majeraha ya kihisia, hasa pale ambapo mifumo ya msaada wa taasisi haipo au haifikiki kwa urahisi.
"Changamoto za afya ya akili ni za kawaida na zinatibika, lakini watu wanahitaji mazingira salama ya kuzungumza waziwazi na kutafuta msaada bila hofu,” alisema.
Ili kushughulikia changamoto hizo kwa muda mrefu, Dkt. Swai alisema kituo hicho kinatarajia kuingiza rasmi mafunzo hayo katika mfumo wake wa kudumu wa mafunzo.
TPTC imejipanga kutoa mafunzo hayo angalau mara tatu kwa mwaka kwa lengo la kujenga uimara wa kisaikolojia kwa walinda amani kutoka mataifa yote yanayochangia vikosi vya ulinzi wa amani.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...