Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imepongeza uamuzi wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Equity For Tanzania (EFTA) kwa kutekeleza mikakati yenye lengo la kuboresha na kuimarisha utendaji wa Kampuni hiyo huku pia mauzo ya Hatifungani yake yakiwa yamepata mafanikio ya asilimia 220.24.
CMSA imeyasema hayo leo Mei 20,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa toleo la kwanza la Hatifungani ya Kampuni ya Equity For Tanzania (EFTA)kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo,viwanda na biashara katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA.Nicodemus Mkama amesema dhamira ya Serikali ni kuona sekta ya fedha inawezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kukuza na kuendeleza biashara zinachangia ukuaji na ustawi wa sekta binafsi, umma na uchumi wa nchi kwa ujumla.
“Hivyo Hatifungani ya EFTA imetoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa dhamira hii, na ni hatua madhubuti ya kuongeza fursa za uwekezaji katika masoko ya mitaji na kuleta matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi yetu.
“Kama tulivyoshuhudia mauzo ya hatifungani ya EFTA yamepata mafanikio ya asilimia 220.24, ambapo kiasi cha Sh.bilioni 33.04 kimepatikana, ikilinganishwa na Sh.bilioni 15 zilizotarajiwa.
“Hatua hii inaiwezesha EFTA kuongeza rasilimali fedha na ukwasi, ambao utatumika kutoa mikopo ya vifaa vya uzalishaji kwa Kampuni ndogo na za Kati za Ujasiriamali (SMEs), kama vile Matrekta na vifaa vya kilimo,Mashine za Kuchakata,magari ya mizigo na utalii, mitambo ya uchimbaji wa madini, vifaa vya ujenzi na mitambo ya viwandani.”
Akieleza zaidi amesema kampuni ya EFTA imeweka historia ya kuwa kampuni ya kwanza katika sekta ya fedha inayotoa huduma ya
ukodishaji wa vifaa vya uzalishaji bila dhamana kuuza hatifungani kwa umma na kupata mafanikio makubwa, na hatimaye hatifungani hiyo inaorodheshwa Soko la Hisa la Dar es Salaam.
“ Hatua hii inaweka msingi imara na inafungua milango kwa kampuni na taasisi zingine katika sekta ya umma na binafsi ambazo zinaonyesha nia ya kutumia fursa katika masoko ya mitaji kupata fedha za kuendesha biashara na kugharamia miradi ya maendeleo.
“Pia hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Serikali wa Njia Mbadala za Kugharamia Miradi ya Maendeleo uliowekwa kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2020/21 – 2029/30 wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo katika sekta ya umma na binafsi,”amesema CPS.Mkama.

Ameongeza kati ya wawekezaji waliowekeza kwenye hatifungani ya EFTA, asilimia 95.4 ni wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 4.53 ni Kampuni na Taasisi.Asilimia 99.4 ni wawekezaji wa ndani wakati asilimia 0.57 ni wawekezaji wa kigeni.
Amefafanua pia kuorodheshwa kwa hatifungani ya EFTA hivi kunaongeza thamani ya uwekezaji katika Hatifungani za Kampuni na Taasisi kwa asilimia 1.66 na kufikia Sh.trilioni 2.03,

kutoka Sh.trilioni 1.99 na ushiriki huo mkubwa wa wawekezaji mmoja mmoja wa ndani ni hatua muhimu katika kuongeza ukwasi katika soko la hisa.
CPA.Mkama amesema hatua hiyo ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Huduma za Kifedha wenye lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye sekta rasmi ya fedha.
“Hivyo, tuna kila sababu ya kuipongeza EFTA pamoja na taasisi na wataalamu wote walioshiriki katika kuwezesha mafanikio haya. Ninatambua kwamba, kazi hiyo haikuwa ndogo na rahisi lakini mmeweza kufanya kazi yenu vizuri.”
Wakati huo huo ametoa mwito kwa kampuni zenye leseni ya kutoa huduma katika masoko ya mitaji kuendeleza mikakati ya kuanzisha bidhaa bunifu zinazopanua na kuongeza fursa kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.
Aidha CMSA itaendelea kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa mikakati yenye lengo la kuchagiza maendeleo ya masoko ya mitaji na hivyo kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...