Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka 2050 unafanikiwa kupitia matumizi ya vipimo sahihi katika sekta mbalimbali za uchumi.

Akizungumza Mei 20, 2026 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani, Londo amesema vipimo sahihi vina mchango mkubwa katika maendeleo ya biashara, kilimo na maisha ya kila siku ya wananchi.

Aidha, amesema Serikali inachukua hatua dhidi ya changamoto ya uuzaji wa mazao kwa mfumo wa “lumbesa”, ambapo watakaa pamoja na Wizara za Kilimo pamoja na TAMISEMI ili kuhakikisha mfumo huo unatokomezwa na wananchi wanazingatia matumizi ya vipimo vinavyokubalika kisheria.

Pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuongeza ufanisi wa huduma na kulinda maslahi ya wananchi dhidi ya udanganyifu wa vipimo.

Kutokana na changamoto hizo, Wakala wa Vipimo kwa kushirikiana na Kampuni ya Climb Up Limited chini ya Mkurugenzi Mtendaji Emmanuel Ngallah imekuja na mfumo maalum wa mizani janja ya kidigitali unaolenga kudhibiti udanganyifu wa vipimo katika biashara mbalimbali.

Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 20, yakilenga kuhamasisha matumizi ya vipimo sahihi kwa manufaa ya jamii na maendeleo ya uchumi.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...