Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha
BENKI ya CRDB imetangaza neema kwa wanahisa kwa ongezeko la asilimia 38 kutoka sh.65 ya mwaka jana hadi kufikia sh.90 kwa hisa moja mwaka huu 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu wa 31 wa wanahisa Leo Mei16, 2026 Jijini hapa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya CRDB Prof. Neema Mori amesema wanahisa wana mchango mkubwa na ni nguzo ya msingi katika maendeleo endelevu.
Aidha amewakaribisha wanahisa kuhudhuria kwa wingi katika semina na mkutano mkuu wa 31 ili kujifunza, kuweka mikakati ya pamoja, kutambua fursa zilizopo, kukaribisha wanahisa wapya na kufahamishwa fursa mpya.
Profesa Neema amesema katika semina watakayoifanya vijana ndio watapewa kipaumbele huku akisisitiza kuwa vijana ndio nguvu ya uwekezaji katika taifa lolote duniani.
"Kupitia semina hiyo vijana wameandaliwa fursa mpya ya uwezeshwaji katika uwekezaji kuhakikisha wanamiliki uchumi mzuri, Mkutano huu ni muhimu sana kwetu, wadau, wanachama na wanahisa kwa ujumla, " amesema.
Amesema kutakuwa na mada 12 za msingi ambazo zitawafanya kufikia mafanikio ya pamoja na kuwataka wanahisa kuendelea kuiamini benki ya CRDB kwa sababu inazingatia misingi na kanuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo imeendelea kuwa imara na kufanikiwa kuvuna faida ya shilingi bilioni 206 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo ameongeza kuwa, ubunifu umeongezeka, na huduma nyingi kwa sasa zinapatikana nje ya benki.
"Mafanikio ya miaka 30 ijayo yanategemea uwekezaji wa kina kwa vijana wa sasa, tutahakikisha tunakuwa nao karibu ili kuandaa wawekezaji wazuri wa kesho.

Benki yetu imevuka mipaka na imeendelea kufanya vizuri kimataifa, nawashukiru sana wateja wetu kutuamini na kuwekeza kwetu, Kama kampuni inayomilikiwa kwa mfumo wa hisa, wanahisa wana nafasi ya kupata taarifa, kutoa maoni na kufahamu mustakabali wa benki yao, Wito wangu kwenu vijana changamkieni fulsa ambazo benki yenu imewaletea ili kesho muwe wawekezaji wakuu wa CRDB" amesema Dkt. Nsekela.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...