Diwani wa Kata ya Ludete, Jumanne Misungwi, amepata chakula cha mchana na watoto waishio katika mazingira magumu,wanaozunguka katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro.

Hafla hiyo ya chakula imefanyika jana wakati wa mkutano wa mwaka wa madereva bajaji katika mji huo.

Mbali na chakula hicho, madereva hao wa bajaji waliweza pia kutoa misaada ya mahitaji mbalimbali katika Kituo cha Watoto Wenye Mahitaji Maalumu cha Katoro Shule ya Msingi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Diwani Misungwi amesema kuwa watoto hao wa mtaani ni sehemu ya jamii na wanapaswa kulindwa ili wajihisi bado jamii inawajali.

Amesisitiza kuwa kila mwanajamii ana wajibu wa kuhakikisha makundi yenye uhitaji yanapata faraja na msaada, badala ya kubaguliwa au kutelekezwa.

Katika siku hiyo muhimu ya waendesha bajaji, Misungwi amewapongeza vijana hao kwa kuandaa tukio hilo lenye kugusa maisha ya wengi.

Aliongeza kuwa kufanya matendo ya huruma na misaada kwa wenye uhitaji kutawawekea baraka katika shughuli zao za kila siku na kukuza mshikamano Katoro.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...