NA MWANDISHI WETU

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imewapongeza walimu wote kwa utekelezaji wa majuku yao kwa mujibu wa sheria na miongozo mbalimbali hususan kulinda haki za watoto na kupambana na ukatili dhidi ya watoto kuhakikisha wanakuwa katika mazingira bora.

Imesema watoto ni kundi ambalo linapaswa kulindwa, kukutetewa zaidi kwa sababu umri walio nao baadhi yao ni vigumu kujisemea, kujitetea au kujilinda dhidi ya ukatili mbalimbali unaoweza kufanywa na jamii inayowazunguka.

Hayo yameelezwa, na Ofisa Mfawidhi wa THBUB Tawi la Dar es Salaam, Shoma Ndono, katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa walimu walezi wa Klabu za Haki za Binadamu mkoani humo.

Shoma, amsemaTHBUB itaendelea kushirikiana kikamilifu na walimu walezi wa klabu hizo za haki za binadamu kuhakikisha zinakuwa imara na endelevu kwa faida ya jamii yote .

“Mafunzo haya yanahusu majukumu ya Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora na kupitia mwongozo wa uendeshaji wa klabu za haki za binadamu shuleni,”ameeleza Shoma.

Amebainisha pia yanalenga kuwawezesha walimu walezi wa klabu hizo kupata maarifa, stadi na mbinu za kulea wanafunzi wawe mabalozi wa haki, amani na utu.

“Mtoto anayejua haki zake anaweza kusimama na kuzitetea pamoja na kuheshimu hazi za wenzake. Pia watoto wafahamu kuwa THBUB ni chombo sahihi kuwasilisha malalamiko yao endapo itaonekana kuwa haiki zao ama za wengine zimevunjwa au zinakaribia kuvunjwa,”amesema ofisa huyo.

Shoma, amebainisha mafunzo hayo ni jukwaa muhimu la walimu walezi wa klabu za haki za binadamu kushirikishana uzoefu na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli zao .

“Kupitia mafunzo haya tunatarajia kupata matokeo na mabadiliko makubwa hivyo kufikia lengo kwani THBUB inawawawezeshaji wazuri na mahiri wa kutoa mafunzo,”amesema.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni walimu kutoka shule za msingi na sekondari mkoani Dar es Salaam, wameeleza mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwao kwani watayafikisha kwa wanafunzi kupitia kalabu za haki.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa, Ashura Kaisinika, ameishukuru THBUB kwa mafunzo hayo abayo yatamsaidia kuwasaidia watoto kufahamu haki zao, kujitetea hususan katika kipindi hiki ambapo vitendo vya ukatili vinaendelea kuchipua katika jamii.

“Mtoto atakuwa alozi mwema kwa jamii yake nay eye atakuwa kiongozi wa taifa baadaye hivyo kutambua haki zinazo stahili,”amesema Ashura.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...