Dkt. Maghembe azindua Kongamano la Vijana wa Kitanzania chini ya Umoja wa Mataifa (TIMUN 2026) asisitiza umuhimu wa nafasi vijana katika kuleta Maendeleo Endelevu Kitaifa na Ulimwenguni

Leo tarehe 18 Mei 2026, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb) amemwakilisha Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye uzinduzi wa Kongamano la Vijana wa Kitanzania chini ya Umoja wa Mataifa (Tanzania International Model United Nations -TIMUN 2026)  linalofanyika Zanzibar. Katika Hotuba yake, Mhe. Naibu Waziri Dkt. Maghembe amesisitiza umuhimu wa nafasi ya vijana katika kuleta maendeleo endelevu na mabadiliko chanya, kupitia teknolojia, diplomasia na ubunifu katika ngazi na Taifa na Ulimwenguni.

Mkutano wa TIMUN 2026, ni jukwaa muhimu la kimataifa linalolenga kukuza viongozi vijana, wanadiplomasia, wabunifu, na mawakala wa mabadiliko ambalo hufanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Chama cha Vijana katika Umoja wa Mataifa Tanzania  (Youth of United Nations Association Tanzania-YUNA).

Mhe. Maghembe ameipongeza YUNA Tanzania kwa kuwawezesha vijana na kuendeleza maadili ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

"Tumieni mkutano huu kubadilishana mawazo, kujenga ushirikiano, na kuibua suluhisho za changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa ajira, usawa wa kijinsia, na maendeleo ya teknolojia" alibaibisha Mhe. Maghembe










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...