Benki ya NMB Plc imepata ufadhili wa jumla ya Dola za Marekani milioni 180, sawa na takribani Sh bilioni 468.1 za Kitanzania, kutoka IFC, British International Investment na Norfund, kwa ajili ya kuongeza mikopo kwa biashara ndogo na za kati, sekta ya kilimo, wanawake wajasiriamali na biashara zinazoongozwa na vijana nchini Tanzania.
Ufadhili huo unajumuisha Dola milioni 100 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa, IFC, sawa na takribani Sh bilioni 260; Dola milioni 50 kutoka British International Investment, BII, sawa na takribani Sh bilioni 130; na Dola milioni 30 kutoka Norfund, sawa na takribani Sh bilioni 78. Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Kigali, Rwanda, pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika, Africa CEO Forum.
Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema ufadhili huo ni ishara ya imani ya taasisi za kimataifa kwa mkakati wa NMB na nafasi yake katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia sekta binafsi, kilimo, wanawake na vijana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi, alisema uwekezaji huo unaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya BII na NMB, huku ukilenga kusaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa MSMEs na biashara za kilimo. NMB inatarajiwa kutumia fedha hizo kuongeza mikopo, kuimarisha minyororo ya thamani ya kilimo na kupanua fursa kwa wajasiriamali nchini.
Hiii apa boss tumia.. Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna (kushoto), na Makamu wa Rais wa IFC Kanda ya Afrika, Ethiopis Tafara, wakionesha hati baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 100 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa NMB kusaidia biashara ndogo na za kati, sekta ya kilimo na maeneo mengine muhimu ya uzalishaji nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna,Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi na Mkurugenzi wa Norfund Kanda ya Afrika Mashariki, William Nyaoke, wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 80 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo utasaidia kuongeza mikopo kwa SMEs, sekta ya kilimo na biashara ambazo hazijafikiwa kikamilifu nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna,Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi na Mkurugenzi wa Norfund Kanda ya Afrika Mashariki, William Nyaoke, wakisaini hati za makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 80 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo utasaidia kuongeza mikopo kwa SMEs, sekta ya kilimo na biashara ambazo hazijafikiwa kikamilifu nchini Tanzania.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Ufadhili huo unajumuisha Dola milioni 100 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa, IFC, sawa na takribani Sh bilioni 260; Dola milioni 50 kutoka British International Investment, BII, sawa na takribani Sh bilioni 130; na Dola milioni 30 kutoka Norfund, sawa na takribani Sh bilioni 78. Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Kigali, Rwanda, pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika, Africa CEO Forum.
Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema ufadhili huo ni ishara ya imani ya taasisi za kimataifa kwa mkakati wa NMB na nafasi yake katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia sekta binafsi, kilimo, wanawake na vijana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi, alisema uwekezaji huo unaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya BII na NMB, huku ukilenga kusaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa MSMEs na biashara za kilimo. NMB inatarajiwa kutumia fedha hizo kuongeza mikopo, kuimarisha minyororo ya thamani ya kilimo na kupanua fursa kwa wajasiriamali nchini.
Hiii apa boss tumia.. Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna (kushoto), na Makamu wa Rais wa IFC Kanda ya Afrika, Ethiopis Tafara, wakionesha hati baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 100 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa NMB kusaidia biashara ndogo na za kati, sekta ya kilimo na maeneo mengine muhimu ya uzalishaji nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna,Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi na Mkurugenzi wa Norfund Kanda ya Afrika Mashariki, William Nyaoke, wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 80 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo utasaidia kuongeza mikopo kwa SMEs, sekta ya kilimo na biashara ambazo hazijafikiwa kikamilifu nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna,Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi na Mkurugenzi wa Norfund Kanda ya Afrika Mashariki, William Nyaoke, wakisaini hati za makubaliano ya ufadhili wa Dola za Marekani milioni 80 pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika jijini Kigali, Rwanda. Ufadhili huo utasaidia kuongeza mikopo kwa SMEs, sekta ya kilimo na biashara ambazo hazijafikiwa kikamilifu nchini Tanzania..jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...