Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kifedha nchini baada ya kuzindua rasmi duka jipya la Yas Store katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kuchochea maendeleo ya kidijitali kwa jamii.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika hivi karibuni, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Yas, Mwangaza Matotola, alisema kufunguliwa kwa duka hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za Yas na Mixx kwa wakazi wa Kunduchi na maeneo ya jirani, hususan katika kipindi ambacho matumizi ya teknolojia yanaendelea kuongezeka kwa kasi nchini.
Alisema Kunduchi ni moja ya maeneo yanayokua kwa kasi kiuchumi na kijamii, huku wananchi wengi wakitegemea huduma za mawasiliano na kifedha katika shughuli zao za kila siku ikiwemo biashara, elimu na ajira za kujitegemea.
“Tunatambua umuhimu wa kuwafikia wananchi pale walipo. Kupitia duka hili, wateja wetu wataweza kupata huduma zote sehemu moja kwa urahisi zaidi,” alisema Matotola.
Aliongeza kuwa uwekezaji wa Yas katika miundombinu ya mawasiliano unaendelea kuleta matokeo chanya kwa Watanzania wengi, ambapo kampuni hiyo imewekeza zaidi ya trilioni moja katika kuboresha mtandao wake kote nchini, ikiwemo ujenzi wa minara zaidi ya 4,800 na upanuzi wa mtandao wa 4G na 5G unaowahudumia zaidi ya wateja milioni 31 nchini.
Kwa mujibu wa Matotola, uwekezaji huo umeendelea kufungua fursa mpya kwa vijana, wafanyabiashara na wanafunzi kwa kuwawezesha kupata huduma za kidijitali kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku.
“Teknolojia si anasa tena, ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Tunapoimarisha huduma za mawasiliano, tunasaidia biashara kukua, vijana kujiajiri kupitia majukwaa ya kidijitali, wanafunzi kupata elimu kwa urahisi zaidi na familia kuendelea kuwasiliana bila vikwazo,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mixx, Arnold Ngarashi, alisema,
“Tunafahamu kuwa huduma za kifedha zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya wananchi wengi, kuanzia wafanyabiashara wadogo hadi vijana wanaojiajiri. Kupitia uwepo wa duka letu hapa Kunduchi, tumejipanga kurahisisha zaidi upatikanaji wa huduma za Mixx na kuwapa wananchi uwezo wa kufanya miamala yao kwa urahisi zaidi bila usumbufu,” alisema Ngarashi.
Aliongeza kuwa Mixx itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata suluhisho za kidijitali zinazowasaidia kukuza biashara zao, kuweka akiba, kufanya malipo na kutuma fedha kwa urahisi zaidi, sambamba na kuchochea ujumuishi wa kifedha nchini.
Sambamba na hilo, Yas imewahimiza wananchi kutumia applikesheni mpya ya Yas App ambayo imezinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kampuni hiyo kidijitali na kufurahia zawadi mbalimbali ndani ya App hiyo.
Wakazi wa Kunduchi waliohudhuria hafla hiyo walieleza kuwa ujio wa duka hilo utasaidia kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano na kifedha, huku wakiamini kuwa hatua hiyo itachochea shughuli za biashara na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma muhimu katika eneo hilo.
Kupitia upanuzi huo wa huduma, Yas na Mixx zinaendelea kuonesha dhamira yao ya kutumia teknolojia kama nyenzo ya kubadilisha maisha ya Watanzania na kuharakisha safari ya taifa kuelekea uchumi wa kidijitali.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas Tanzania, Bi. Mwangaza Matotola (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya la Yas lililopo Kunduchi, Dar es Salaam, hivi karibuni. Wanaoshuhudia tukio hilo ni, kulia ni Mkuu wa Maduka wa Yas Tanzania, Bi. Sarah Sonelo pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji wa Huduma kwa Wateja, Bw. Henry Mboya (kushoto). Duka hilo jipya linalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa wakazi na wafanyabiashara wa Kunduchi na maeneo ya jirani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...