KOCHA BINGWA WA MICHEZO YA UOGELEAJI AUSTIN PILLADO ATUA DAR, KUWEKA KAMBI SIKU 10
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaamHATIMAYE Kocha maarufu kutoka Marekani, Austin Pillado ambaye pia ni Naibu Kocha Mkuu wa timu ya kuogelea kutoka Chuo Washington State, ametua nchini jana Jumapili kwa ajili ya kuendesha kambi maalumu ya mafunzo ya kuogelea kwa muda wa siku 10.
Kambi hiyo inayofanyika jijini Dar es Salaam, imeandaliwa na Shule ya Kimataifa ya Monti kwa kushirikiana na Chama cha Mchezo wa Kuogelea Nchini (TSA).
Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya kocha huyo kwenye uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu na Mwanzilishi wa shule hiyo ya Monti International, Fatma Fernandes alisema lengo kuu ni kuinua viwango vya vipaji vya ndani kufikia hadhi ya kimataifa.
“Hii ni siku ambayo tunaanza hatua muhimu ya kuinua michezo ya kuogelea na maendeleo ya vijana hapa nchini Tanzania.
“Kwa sababu mpango huu wa mafunzo ya kambi maalumu ya kuogelea unaendana kikamilifu na maono ya uongozi wetu wa kitaifa kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza vipaji vya vijana, hadi kwa Waziri Habari, Sanaa na Michezo, Paul Makonda katika kuhakikisha michezo yote inapewa nafasi ya kukua.
“Sisi Monti International tunaamini kuogelea kunaweza kuwa nguzo muhimu ya michezo Tanzania, na sekta binafsi ina nafasi kubwa ya kuchangia katika kujenga mafanikio hayo,” amesema Fatma.
Naye Mwenyekiti wa TSA, David Mwasogye amesema ujio wa kocha huyo kutasaidia kupunguza au kuziba pengo kati ya vipaji vya ndani na viwango vya kimataifa.
“Kwa kuwaleta makocha wa kiwango cha juu kama Austin, tunawezesha vijana wetu kupata mafunzo na uchambuzi wa kitaalamu sawa na wanariadha bora duniani,” alisema Mwasogye.
Aidha, Kocha Austin Pillado mbali na kupongeza utayari wa Watanzania kujifunza na kupokea changamoto mpya, alisema Tanzania ina vipaji vingi lakini vinahitaji kupewa fursa ya kupata mafunzo ya kiwango cha juu cha kushindana kimataifa.
“Ndiyo maana nimekuja hapa Tanzania kubadilishana uzoefu kutoka kwenye mfumo wa kimataifa wa NCAA, lengo ni kuona watoto na wakufunzi wanapata mafunzo yenye viwango sawa na wanamichezo bora duniani.
Kocha maarufu kutoka Marekani, Austin Pillado ambaye pia ni Naibu Kocha Mkuu wa timu ya kuogelea kutoka Chuo Washington State (katikati) akiwa ameshika bendera ya Tanzania sambamba na Mkurugenzi mkuu na Mwanzilishi wa shule hiyo ya Monti International, Fatma Fernandes (kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasogye (kulia). Austin amekuja nchini kuongoza kambi ya siku 10 ya mafunzo maalumu ya kuogelea jijini Dar es Salaam.
Kocha maarufu kutoka Marekani, Austin Pillado ambaye pia ni Naibu Kocha Mkuu wa timu ya kuogelea kutoka Chuo Washington State na Mkurugenzi mkuu na Mwanzilishi wa shule ya Monti International, Fatma Fernandes (kushoto) wakicheza pamoja na wasanii katika mapokezi yake jijini Dar es salaam. Austin amekuja nchini kuongoza kambi ya siku 10 ya mafunzo maalumu ya kuogelea jijini Dar es Salaam.

.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...