Na Karama Kenyunko,Michuzi TV.
SERIKALI ya Tanzania na Kenya zimesaini mikataba nane ya makubaliano yenye lengo la kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo katika nchi hizo mbili
Hafla ya utiaji saini mikataba hiyo imefanyika leo Mei 4, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam baina ya mawaziri na watendaji wa sekta husika, ikishuhudiwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hasaan na Rais wa Kenya William Ruto ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mkataba wa kwanza uliosainiwa ni hati ya makubaliano kuhusu ushirikiano wa uendelezaji na usimamizi wa reli kati ya serikali ya Tanzania na Kenya, na wa pili unahusu upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa.
Mkataba wa tatu ni kuhusu usaidizi wa kisheria katika masuala ya jinai kati ya serikali hizo mbili na wa nne ni makubaliano kuhusu masuala ya kilimo kati ya Tanzania na Kenya huku wa tano ukihusu utambuzi wa vyeti vya mabaharia.
Mkataba wa sita ni hati ya makubaliano wa kuimarisha uhusiano na usimamizi wa sekta ya usafiri wa njia ya maji , mkataba wa saba ni ushirikiano kati ya taasisi ya viwango Zanzibar na shirika la viwango la Kenya.
Pia wa nane ukiwa ni hati ya makubaliano kati ya vyuo vya utumishi wa umma vya Tanzania na Kenya kuhusu kujengeana uwezo katika masuala ya utumishi wa umma ambapo mikataba hiyo minane ilielezwa kuwa ishara ya ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya Tanzania na Kenya.
Kuhuzu ziara ya kiongozi huyo, Rais Dkt.Samia amesema kuwa ziara ya Rais Ruto imekuwa ya kiserikali na imelenga kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kujadili maendeleo na uwekezaji.
“Rais wa Kenya mara nyingi amekuwa akija Tanzania kwa shughuli mbalimbali, lakini leo amekuja kwa ziara rasmi ya kiserikali.
“Katika ziara hii tumefanya mazungumzo muda mfupi uliopita kuangalia maendeleo ya nchi zetu lakini pia tumezungumza masuala ya siasa na ulinzi na kukuza uwekezaji katika nchi zetu,” amesema Rais Dk.Samia.
Aidha, Rais Samia ameeleza kuwa wamekubaliana katika miradi ya maendeleo ikiwemo bomba la gesi pamoja na sekta ya uchukuzi na miundombinu.“Tumekubaliana pia kuhusu bomba la gesi kutoka Tanzania Dar es Salaam kuelekea Mombasa Kenya na kama mlivyoshuhudia tumesaini maelewano.
“Pia kwenye uchukuzi na miundombinu tumekubaliana kwenye reli kutoka Bandari ya Tanga itapita Kilimanjaro hadi Kenya na usafiri wa ndani ya maji katika maziwa yetu hasa Ziwa Victoria kuunganisha biashara ya Kenya na Tanzania,” amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba 8 ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya katika sekta mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 04 Mei, 2026. Mikataba 8 iliyosainiwa ni kuhusu masuala ya usimamizi wa Reli, upembuzi yakinifu wa mradi wa bomba la Gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, usaidizi wa Kisheria kuhusu masuala ya jinai, masuala ya Kilimo, utambuzi wa vyeti vya Mabaharia, usimamizi wa sekta ya Usafiri kwa njia ya maji, masuala ya Viwango pamoja na kujengeana uwezo kwenye masuala ya Utumishi wa Umma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...