-Ni zilizoingizwa kinyume na utaratibu ili kwenda kutengeneza dawa za kulevya
-DCEA yaweka wazi jinsi walivyozikamata,magari yaliyokuwa yakizisafirisha yashikiliwa
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
OPERESHENI maalum iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya jijini Dar es Salaam imewezesha kukamatwa kwa lita 66,048 za kemikali bashirifu zilizoingizwa nchini kinyume na taratibu za kisheria.
Katika operesheni hiyo iliyofanyika Aprili mwaka huu,Mamlaka hiyo imeshirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Akizungumza leo Mei 13,2025 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amezitaja kemikali zilizokamatwa ni Cyclohexanone zenye ujazo wa lita 16,048 na Extra Neutral Alcohol (ENA) zenye ujazo wa lita 50,000.
Aidha amesema magari mawili yaliyohusika kusafirisha kemikali hizo yanashikiliwa na watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
“Kutokana na udhibiti wa dawa za kulevya kuimarika duniani, mitandao ya kihalifu imekuwa ikitumia kemikali bashirifu kuzalisha dawa za kulevya katika maabara bubu.
“Kemikali hizo ni halali kwa matumizi ya viwandani, kitabibu, kilimo, ujenzi, madini pamoja na tafiti za kisayansi, lakini wahalifu huzitumia vibaya kwa kuzichepusha kutoka katika matumizi halali na kuzitumia kutengeneza dawa za kulevya.”
Ameongeza hali hiyo imeongeza changamoto katika mapambano didi ya dawa za kulevya duniani na kuifanya nchi yetu kuendelea kumarisha mifumo ya udhibiti wa kemikali bashirifu ili kuzuia uchepushwaji wake katika matumizi haramu.
Kamishina Jenerali Lyimo amesema uchunguzi ullofanyika umebaini kemikali aina ya Cyclohexanone zillingizwamnchini na kampuni ya Kinglion Investment Company LTD kinyume na mataka ya mitumo ya udhibiti ikivemo kibali kutoka Mamaka husika.
Adha, kemikali aina ya Extra Neutral Alcohol (ENA) zilikuwa zinasafirishwa kwa kutumia magari ya yanayotumika kubeba mafuta aina ya Petroli yaliyoandikwa Danay Petroleum 3YE 1203 aina ya Scania kwa utumia vibali wya kughushi.
“Magari mayo yalkuwa yakibeba kemikali kutoka kampuni ya Maranie Group Company Limited iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani.”
Amesema katika operesheni hiyo, Mamlaka imemkamata Bakira Abel Zacharia (44), mkazi wa Dar es Salaam, dereva wa gari namba T 794 BMB lenye tela tanki namba T 166 AHW lililokuwa limebeba lita 30,000 za kemikali hizo.
Pia, mamlaka imemkamata Vicent Stephen Rashid (26), mkazi wa Mbeya, dereva wa gari namba T 568 EQF lenye tela tanki namba T 640 EQN lililokuwa limebeba lita 20,000 za kemikali hizo.
“Mazingira ya uingizaji na usafirishaji wa kemikali hizo yanaashiria uwepo wa nia ovu ya kuzichepusha kwa matumizi haramu, ikiwemo utengenezaji wa dawa za kulevya.
“Kemikali aina ya Cyclohexanone ni miongoni mwa kemikali zilizothibitika kimataifa kutokana na taarifa za kutumika katika maabara bubu zinazozalisha dawa za kulevya aina ya Phencyclidine (PCP).”
Aidha, lita 16,048 za kemikali za Cyclohexanone zilizokamatwa kama zingechepushwa zingeweza kuzalisha tani 11.4 za dawa za kulevya aina ya Phencyclidine kwa kuwa kilo moja ya kemikali hizo huweza kuzalisha takribani gramu 750 za dawa za kulevya.
Amefafanua kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani sura 182, usafirishaji wa kemikali unahitaji taratibu maalumu ikiwemo vibali vya kuingiza na kusafrisha Kemikali.
“Matumizi ya vibali vya kughushi na utoaji wa taarifa za ongo kuhusu matumizi yaliyokusudiwa ya kemikali husika ni kosa kisheria,”amesisitiza.
Pia amesema usafrishaji wa kemikali kwa nja fiche hususani kwa kutumia magari ya kubeba petroli ni ukukwaji mkubwa wa taratibu za udhibiti wa kemikali na ni kiashiria cha uwepo wa jaribio la kuzichepusha kwa matumizi haramu.


.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...