Mageuzi ya biashara ya mazao nchini yanaendelea kushuhudiwa kupitia ushirikiano kati ya COPRA na Bodi ya Stakabadhi za Ghala (WRRB).
Akizungumza katika warsha kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi. Irene Mlola, amesema matumizi ya mfumo wa mauzo kidijitali unaojumuisha Mfumo wa Stakabadhi Ghalani yameendelea kurahisisha biashara ya mazao, kuongeza fursa za masoko na kunufaisha wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani.
Mafanikio mengine yaliyochagizwa na COPRA kupitia mfumo huo ni pamoja na;
Kuongezeka kwa bei ya mazao kwa wakulima kwa wastani wa asilimia 15 - 30, Wakulima kunufaika na asilimia 75 hadi 80 ya bei ya soko la dunia kwa mazao mbalimbali, Kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya mazao kwa zaidi ya asilimia 30, Kuongezeka kwa thamani ya biashara ya mazao kutoka shilingi bilioni 896 hadi trilioni 1.4, asilimia 94 ya mapato ya mazao ya mbaazi, choroko, dengu na ufuta kwenda moja kwa moja kwa wakulima.
Bi. Mlola ameeleza mafanikio mengine ni kuongezeka kwa mapato ya kodi katika sekta ya kilimo kutoka shilingi bilioni 26 hadi bilioni 40, kupanuka kwa masoko ya kimataifa pamoja na kuongezeka kwa matumizi ya minada ya kidijitali na huduma za kifedha kwa wakulima.
Aidha, Bi. Mlola ameipongeza WRRB kwa kuadhimisha miaka 20 ya huduma na kuahidi kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...