Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

DIWANI wa Kata Kariakoo Haji Manara ametoa ombi malaamu kwa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi wa Jiji hilo kuja na ajenda maalum ya kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi kuelekea michuano ya AFCON.

Tanzania na hasa Jiji la Dar es Salaam imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa michuano ya AFCON hivyo matarajio kutakuwa na maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali,hivyo kuwa na ajenda ya kudumu kwa ajili ya kuliboresha Jiji hilo ni muhimu ikawa ya kudumu kuanzia sasa.

Akiwasilisha maombi maalum katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika leo Mei 14,2026 ,Manara ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Mkurugenzi wa Jiji na Meya kuhakikisha Jiji linakuwa safi.

“Mungu akitujaalia mwakani Tanzania  itakuwa mwenyeji michuano ya AFCON na ufunguzi utanyika jijini Dar es Salaam na kutakuwa na mechi zitakzochezwa Dar es Salaam.Hivyo naomba tuwe na ajenda ya kudumu itakayokuwa inajadili kwa kushirikiana na kamati ya maandilizi na serikali yetu

“Sura ya Dar es Salaam inaendelea kupendeza lakin lazima tufanye jitihada za kuhakikisha Jiji linakuwa safi kwani itakuwa aibu kuwa na Jiji  chafu,mitaro kujaa maji, lakini kuwa na misongamano isiyokuwa na ulazima.

“Pia kuelekea AFCON lazima tuandae watu wa kupokea wageni,hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Sslaam nakuomba ubebe ajenda hii.Jiji la Dar es Salaam kuna Hoteli zenye hadhi ya Five Star tano ambazo zinaweza kupokea maelfu ya wageni.”

Akifafanua zaidi Manara amesema pamoja na uwepo wa hoteli hizo iko haja kwa Mkurugenzi pamoja na Meya kuangalia uwezekano wa kuzungumza na wamiliki wa Apatiment ili ziweze kupokea wageni kwani wapo watakaotoka mikoani ambapo sio wote wanaweza kufikia kwenye hoteli kubwa,hivyo watafikia kwenye apatimenti ziliozopo.

“Naomba tuzungumze na wamiliki wa Apatiment kwa ajili ya kupokea wageni,kwani sio watu wote ambao wataweza kukaa Hayat Regency na hoteli nyingine kubwa za namna hiyo, hivyo wengine watakaokuja watakaa huko,”amesema Manara.

Wakati huo huo amesema kwa upande mwingine Jiji la Dar es Salaam limekuwa nyuma katika utalii hivyo iko haja ya kuwa na kumbi maalum ambazo zitakuwa zinatumika katika utalii katika kipindi ambacho michuano ya AFCON itakuwa inaendelea.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...