Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilali maarufu Shetta amesema anatambua na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Baraza la madiwani pamoja na watumishi wote wa halmashauri hiyo.
Aidha amesema kutokana na ushirikiano baina ya viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni wazi wataendelea kutekeleza majukumu yao na kubwa zaidi ni kuifanya halmashauri hiyo kuwa namba moja nchini katika kukusanya mapato.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Mdiwani Robo 3 ya mwaka 2026 kuanzia Januari hadi Machi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichokutana kujadili taarifa za utendaji kazi wa kata za Halnashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
“Naomba kutambua kazi nzuri inayofanywa na kila mmoja wetu katika halmashauri yatu na viongozi wa kitaifa wamekuwa wakipongeza baraza letu kwa kazi nzuri inayofanyika,ukweli tunapokea sifa nyingi.
“Tuendelee kuwa halmashari namba moja katika kukusanya mapato,kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuilete heshima nchi yetu pamoja na kumletea heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Katika kikao hicho pia Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeshuhudia Diwani Mteule wa Viti Maalum Gema Ishengoma akila kiapo cha kuwa Diwani ambapo Meya Bilal ametumia nafasi hiyo kumkaribisha huku akiomba madiwani na watumishi wa Jiji hilo kumpatia ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake kwa maendeleo ya wananchi.
“Chama Cha Mapinduzi(CCM)kama kilivyokuwa ltanuru la kupika viongozi kuanzia jumuiya ya chipukizi basi hata diwani aliyekuja atatusaidia katika baraza la halmashauri na kubwa zaidi tutampa ushirikiano ili apate nafasi ya kufanya kazi vizuri

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...