Na Nasra Ismail, Geita
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, amemwagia sifa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Mkoa wa Geita, Gervas Evarist, akimtaja kama mhimili muhimu katika kuimarisha chama mkoani humo kupitia uboreshaji wa miundombinu.
Akizungumza kwenye mikutano ya shukrani kufuatia ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, Dkt. Biteko alibainisha kuwa mchango wa kifedha wa MNEC Evarist umewezesha ujenzi wa ofisi za kisasa katika kata mbalimbali, hususan wilayani Bukombe.
Alieleza kuwa hatua hiyo ni kielelezo cha uongozi unaojali hadhi ya chama.Katika ziara hiyo iliyopita kwenye kata za Bulega, Bugelenga, Iyogelo, na Ng’anzo, Dkt. Biteko aliambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Matondo Lutondo, ambapo alijionea miradi mbalimbali ikiwemo majengo ya biashara na nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na chama.
"Viongozi wanapimwa kwa kazi na si maneno. Uwepo wa ofisi bora na miradi ya kiuchumi ni siri ya utulivu na mafanikio ya chama chetu katika ngazi ya kata," alisisitiza Dkt. Biteko.
Mbali na masuala ya chama, Dkt. Biteko aliahidi kutoa mabati kwa ajili ya Zahanati ya Mtinga, huku Mwenyekiti wa Halmashauri, Erick Kagoma, akiwahimiza wananchi kuchangamkia mikopo ya 10% ya halmashauri ili kujiletea maendeleo.



.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...