Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2026 Wazo Mwang'onda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Bohari yenye urefu wa mita 600 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika mtaa wa Bohari Kata ya Mwenge Manispaa ya Lindi wenye thamani ya zaidi ya milioni 466
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Leo Mei 2, 2026 Mwang'onda amewapongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo ambao utachochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Awali akisoma taarifa mbele ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2026 Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Mhandisi Downson Paschal amesema Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Mafuta utekelezaji wake umefikia asilimia 90.
Amesema mkandarasi anayetekeleza mradi huo ni kampuni ya SEC ya Mtwara, ambapo ujenzi ulianza Septemba 20, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mei 28, 2026 ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa hadi sasa kazi mbalimbali zimekwisha fanyika ikiwemo kusafisha eneo la barabara, kujenga tabaka la msingi pamoja na uwekaji wa mifereji na makalavati ili kuhakikisha barabara hiyo inadumu kwa muda mrefu.
Aidha amebainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, kupunguza changamoto ya vumbi pamoja na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wakazi wa Kata ya Mwenge wa Uhuru na maeneo jirani.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa hiyo ya Lindi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo ya miundombinu, huku wakibainisha kuwa hatua hiyo imesaidia kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.
.jpeg)


.jpeg)


.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...